Mgombea wa nafasi ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kilangala, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Jenga Mohamedi na wajumbe saba wa Mkutano Mkuu wa kata wa chama hicho wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakidaiwa kupokea na kutoa rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 18, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Steven Chami amesema watu nane wamekamatwa akiwamo Mgombea ukatibu aliyekutwa akitoa rushwa kwa wajumbe ili achaguliwe.
Kwa mujibu wa Chami, tukio hilo limetokea jana saa mbili asubuhi kwenye eneo la uchaguzi huku watuhumiwa wakiwa na fedha Sh 2,000 kila mmoja huku mpambe wa mgombea huyo alikutwa na bulungutu kiasi hicho cha fedha zenye thamani ya Sh 50,000 na orodha ya majina ya wajumbe wa mkutano huo.
Alisema watuhumiwa wanashikiliwa na Taasisi hiyo hadi mahojiano yatakapo kamilika na hatua zingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yao
0 comments :
Post a Comment