Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally amesema hataonekana katika majukwaa ya siasa kwa sababu yeye ameteuliwa kuwa mtendaji na si mwanasiasa wa chama hicho hivyo atatekeleza yale tu yanayoamriwa katika vikao vya Halmashauri Kuu.
Dk. Bashiru amesema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa ofisi na kutambulishwa kwa watendaji wa chama hicho, na Katibu Mkuu mstaafu, Abdulrhaman Kinana katika Ofisi kuu za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.
“Mimi nimeteuliwa kuwa mtendaji wa chama kazi niliyopewa si ya jukwaaani, ni marufuku kwa watendaji kujihusisha na siasa hivyo watu wasitarajie kuniona katika majukwaa.
“Jukumu langu kubwa ni kutekeleza maazimio ya vikao, kutoa taarifa pamoja na kusimamia maagizo ya chama haya ni masuala ya mezani si ya jukwaani wapo waliopewa dhamana ya kukaa katika majukwaa,” alisema Dk. Bashiru.
Aidha, alisema atalipa kipaumbele suala la serikali kuhamia Dodoma ambapo katika miaka iliyopita walishindwa, hivyo ataanzia hapo na kuhakikisha wanafanikiwa na ataendelea pale walipoanzia
0 comments :
Post a Comment