Mambo 6 Yakuzingatia Wakati wa Kuchagua na Kusajili Jina la Website yako au ya Kampuni yako

Je umeshawahi kufikiria ni jinsi gani watu wananyohangaika kufika mtaani kwenu kama huo mtaa jina lake halieleweki?

Majina ya Website ama kwa kingereza wanaita "Domain Names", kama ilivyo anuani za mitaa au nyumba zina maana kubwa sana kwenye ulimwengu wa Website. 

Uchaguzi wake ni moja ya vitu muhimu sana katika maisha ya website, jina lisiloeleweka, siyo tu litaweza kumpa faida mpinzani wako, bali kuwachanganya wateja na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wako kwenye mtandao.

Kabla hatujaendelea, lazima tujue ni kwa nini kuna majina ya website?

 Inteneti ni netiwoki ya kompyuta ambazo zimeunganishwa na zina uwezo wa kuwasiliana kwa kutumia kanuni za inteneti ( Intenet Protocol ) .

Ili mashine hizi ziwasiliane zinatakiwa zijuane, sawa na sisi tunavyojuana huko mitaani. Kwa machine hizi zinatumia namba zinazoitwa IP (mfano: 123.12.121.11) kama utambulishi wa mashine kwenye intaneti. Kwakuwa ni ngumu sana kukumbuka lundo la hizi namba, hapo ndipo majina ya website yalipoibuka.

Majina haya ni herufi zinazosomeka zikiwa ni njia mbadala wa kuwasilisha IP. 

Kwa mfano, mtu unapoandika mpekuzihuru.com, website inawasiliana na mahali hii domain ilipofunguliwa ili kuulizia IP yake, hivyo kwa mashine, zao zinatumia IP ila sisi binadamu tunatumia majina wya website. Kwa maneno mengi, majina haya ni kwa ajili ya kurahisisha matumizi kwa binadamu na siyo kwa ajili ya mashine.

Baada ya kuona historia fupi ya majina haya, hebu tuangalie ni vitu gani unatakiwa kuzingatia wakati unachagua majina ya website.
 
1.Liwe na Mvuto.
Mvuto wa jina ni kitu cha kwanza kabisa, jaribu jina litakalokueleza moja kwa moja. Kwa mfano, wewe unafanya biashara ya nguo, ukiwa na webiste yenye jina la nguobomba.com au nguonzuri.com ni dhahiri kuwa mtu akifika tu anajua hii ni website ya nguo tena zilizo bomba.

Hakuna kujiuliza mara mbili utakuwa umeua ndege wawili kwa pamoja, umetangaza biashara ya nguo na umejipa taswira ya nguo bomba na hicho nicho kitu cha muhimu kwenye biashara za mtandaoni. Ingawa majina mengi mazuri tayari yameshachukuliwa, lakini unaweza kufanya utafiti zaidi.
 
2. Lisilochanganya herufi, uwingi na pia linatamkika kiurahisi.
Epuka kutumia uwingi, kwa mfano kwakuwa ciscotechnology.com limeshachukulia, ukaja na jina kama ciscotechnologies.com ni dhahiri kwa wengi wataishia kwenye umoja na hii ndiyo hulka ya binadamu. Kama jina unalolitaka limeshachukuliwa, usijaribu kulazimisha kwa kuongeza maneno au uwingi. Umiza kichwa njoo na jina la kipekee na lenye mvuto.
 
3. Liwe fupi na lisilo na mkanganyiko wa maneno.
Je ushawahi kuona majina kama businessssimplewaytanzania.com, na walengwa wake ni Watanzania? Jina kama hili siyo tu ni refu mno, bali pia lina mkanganyiko wa maneno mengi mno. Jina kama hili halikumbukiki kiurahisi, na pia ni ngumu kukaririka. 
 
4.Liilinde brandi yako
Hii imeshawahi kutokea mara nyingi sana, jina la website liwe linaloweza kusimama na kuelezea brandi yako. Siyo lazima jina la website liwe sawa na jina la kampuni, kwa mfano, Huawei Technologies kama wangetumia huaweitechnologies.com basi ingekuwa ni ngumu sana ao kukumbukika

Angalia pia watu kama Google, Yahoo! na Facebook. Wamefanikiwa na majina ya website zao zinawakilisha brand yao moja kwa moja.
 
5. Tumia viendelezo husika
Ingawa .com, .co.tz na .net ni moja ya majina ambayo yanatumika sanasana, ila kuna viendelezo vingine vingi ambavyo unaweza kutumia. 

Kitu cha msingi ni kuwa, hakikisha unajua website yako inaangukia kwenye kundi gani, website ya shule inapendeza wakatumia .ac.tz badala ya .co.tz. Kwakuwa .com ni kiendelezo kinachotumika kwa wingi, hivyo hakikisha website yako inamiliki .com. 

6.Hakikisha unanunua toka kwa kampuni inayoeleweka
Hakikisha kampuni unayonunua jina inaeleweka na ina picha nzuri kwa jamii inayoihudumia. Kwa kufanya makosa kwenye jina kunaweza kukugharimu kiasi kikubwa na hata kusababisha website isiwe hewani kwa miezi. Siyo kila muuza jina ni wa kumuamini. Akiwa ndiye mtu anayehifadhi jina lako, hakikisha unawafahamu vyema na unajua utendaji wao.

Kama una ndoto ya kumiliki website, nakushauri utumie Hostigator....Ni kampuni inayojielewa na bei zao ni nzuri

<<INGIA HAPA>>  Uanze kumiliki website yako Leo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment