RYAN
Giggs ameanza vizuri kazi yake akiwa meneja wa muda wa Manchester
United baada
ya kuilaza Nowrich City mabao 4-0 katika mechi ya ligi kuu
soka nchini England kwenye uwanja wa Old Trafford.Wayne Mark Rooney amefunga mabao mawili, huku Juan Mata aliyeanzia benchi leo hii naye akifunga mabao mawili.
Giggs ambaye kwa muda mrefu ameitumikia klabu ya Man United akiwa mchezaji, aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda baada ya David Moyes kufukuzwa kazi jumanne ya wiki hii.
Matokea ya leo ni mabaya mno kwa Nowrich City kwasababu yanawaweka katika hatari ya kushuka daraja, huku wakibakiwa na mechi ngumu dhidi ya Asernal na Chelsea.
Man United wanabakia nafasi yao ya 7 kwa kujikusanyia pointi 60 baada ya kucheza mechi 35.
Rooney baada ya kuchangia ushindi wa leo amesema kuwa anaamini Giggs ana kila sifa ya kuwa meneja wa kudumu wa Manchester United.
“Ilikuwa tofauti kabisa leo chini ya Giggs”. Rooney ameuambia mtandao wa Sky Sports.
“Nimecheza naye kwa miaka 10, lakini wote tunajua kuwa ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na amekuwa sehemu ya benchi la ufundi msimu uliopita”.
“Anajijenga kuwa kocha. Sisi kama timu tunaona hilo”
“ Tunaona jinsi alivyoanza majukumu yake baada ya kuteuliwa”
“ Imekuwa furaha kupata ushindi mbele yake”. Amesema Rooney muda mfupi baada ya mechi kumalizika.
Rooney ameongeza kuwa kila kitu kipo chini ya bodi kwasababu wao ndio wenye mamlaka ya kuchagua nani kuwa kocha mkuu na hakuna anayejua, lakini Giggs anastahili kushika nafasi hiyo.
“Kwa upande wangu ninajisikia furaha kufanya kazi chini yake”.
“Tangu nikiwa mdogo, nakumbuka alikuwa anacheza.”
“ Ni mtu mzuri wa Man United. Unaweza kusema alizaliwa hapa na nadhani wachezaji wote wanajisikia vizuri kuwa naye katika mazoezi”.
“Lakini lipo juu ya uwezo wetu, maamuzi ni juu ya bodi. Acha tufurahi tukiwa naye mpaka mwisho wa msimu”. Alisema Mata
0 comments :
Post a Comment