Saturday, June 27, 2015
Nkupamah blog
MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), amemuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kudai aielekeze Serikali kuleta ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za ununuzi wa mabehewa kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Kafulila alisema mbali na
barua hiyo, pia ataendelea kulizungumzia suala hilo bungeni hadi ripoti
hiyo itakapoletwa bungeni.
Alisema
jambo hilo ni nyeti kwa kuzingatia kuwa taarifa ya awali ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA), ilibainisha wazi kuwa ununuzi wa
mabehewa hayo uliofanywa na Kampuni ya Hidustan ya India ulikuwa na
mapungufu.
“Mapungufu
hayo ni pamoja na mabehewa kutozingatia viwango vilivyohitajika, kwa
maana kulikuwa na udhaifu katika ‘Specifications’ na utangazaji zabuni
ya mabehewa hayo. Wizara ya Uchukuzi haikuhakikisha uchunguzi wa uwezo
na rekodi za kampuni kabla ya kupewa zabuni hiyo.
“Wizara ya Fedha ilifanya malipo mapema kinyume cha taratibu kabla ya mabehewa kufikishwa nchini,” alisema Kafulila.
Alisema
Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, alikiri kwamba alishapokea ripoti
hiyo, hivyo haoni sababu ya kutokuletwa kwa taarifa ya utekelezaji wake
bungeni ili ijadiliwe na wabunge.
Alisema jambo hilo ni kubwa na linahusu uhai na gharama ya Sh bilioni 238.
Wakati
Sitta akijibu hoja za wabunge wakati wa bajeti ya Wizara yake alisema
watu watano wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na ufisadi huo.
Alisema
kamati ya uchunguzi katika taarifa yake ilibaini kuwepo kwa makosa ya
uzembe, hali iliyosababisha hasara ya Sh bilioni 12 na si Sh bilioni 238
kama inavyodaiwa.
Kamati
iliyoundwa kuchunguza sakata hilo iliihusisha Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mwanasheria Mkuu (AG), Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wahandisi.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment