Alipowasili
Ethiopia, Julai 26, 2015, rais wa Marekani Barack Obama (kulia)
amekaribishwa na Waziri mkuu Hailemariam Desalegn na mkewe (kushoto)
Na RFI
Rais wa
Marekani Barack Obama amewasili nchini Ethiopia Jumapili usiku katika
ziara ya kikazi ya masaa 48. Ikiwa ni kwa mara ya kwanza rais wa
Marekani kufanya ziara nchini Ethiopia, Barack Obama anaitambua Ethiopia
kama mshirika muhimu katika vita dhidi ya ugaidi katika Pembe ya
Afrika.
Hata hivyo Ethiopia ni nchi ambayo imeendelea kuvunja na kukiuka haki za binadamu.
Barack
Obama yupo mjini Addis Ababa kwa muda wa siku mbili. Jumatatu asubuhi
wiki hii, atakuwa na mazungumzo na Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam
Desalegn, pamoja na rais Mulatu Teshome, ambaye ana majukumu ya kimfano.
Pamoja na
ukuaji wake wa kiuchumi wenye kuvutia na raia wake zaidi ya milioni 90,
Ethiopia kwa sasa imekua nchi yenye kuvutia barani Afrika. Suala la
usalama litagubika mkutano kati ya Barack Obama na viongozi wa taifa
hilo.(P.T)
Mkutano
kuhusu hali inayojiri nchini Sudan Kusini na vita dhidi ya ugaidi
unatazamiwa kuanza leo Jumatatu mchana. Wanamgambo wa kiislamu wa Al
Shebab wamethibitisha kwamba wangeweza kuendesha mashambulizi na
mikutano mbalimbali imeendelea kufanyika ili kupata ufumbuzi kwa vita
vya wenyewe kwa vinavyoendelea kushuhudiwa nchini Sudan Kusini.
Hali hizi
mbili ni zitajadiliwa zaidi katika mkutano huo unaosubiriwa kwa hamu na
gamu Jumatatu wiki hii mchana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Lakini kwa ujumla, eneo la Kaskazini Mashariki mwa Afrika bado
linakabiliwa na vurugu ambapo Marekani bado ina washirika waaminifu.
Ethiopia imewatuma wanajeshi wake kujiunga katika kikosi cha Umoja wa
Afrika nchini Somalia, lakini pia katika mstari wa mbele katika
upatanishi juu ya Sudan Kusini, na hivyo kuwa mshirika wa karibu wa
Marekani.
Haki za binadamu katika mpango mbadala?
Kando na
mikutano iliyopangwa, ziara ya Barack Obama inaweza pia kutafsiriwa kama
ishara ya kuunga mkono utawala wa Ethiopia. Utawala ambao umeendelea
kusalia madarakani kwa miaka mitano mfululizona kujipatia 100% ya viti
Bungeni. Pia utawala ambao, mbinu inazotumia zimekua zikikosolewa na
mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini humo na kungineko duniani.
Katika
mazingira haya, je rais wa Marekani atajitolea ili kuwapa nasaha
viongozi wa nchi hiyo kuheshimu misingi ya demokrasia na uhuru wa
kujieleza? Huenda akajizuia kutoa nasaha hiyo katika hotuba atakayoitoa
mbele ya Umoja wa Afrika Jumanne wiki hii.
0 comments :
Post a Comment