Na Faustine Ruta, Bukoba
Shirika
lisilokuwa la serikali la Friends of Children with Cancer Tanzania
(FOCC TZ) lazindua rasmi huduma ya upasuaji wa watoto wenye ugonjwa wa
vichwa kujaa maji na mgongo wazi mkoani Kagera katika Hospitali ya Rufaa
ya mkoa ambapo jumla ya watoto arobaini wenye tatizo hilo wanatajiwa
kufanyiwa upasuaji kuanzia Julai 25-26, 2015.
Mkurugenzi wa shirika la FOCCTZ Bw. Walter Miya katika uzinduzi huo
alisema kuwa baada ya kutoa matangazo kupitia redio za jamii mkoani
Kagera kwa muda wa siku mbili wameweza kupata watoto 70 wenye tatizo la
vichwa kujaa maji na mgongio wazi kutoka katika wilaya zote saba za mkao
wa Kagera na nje ya mkoa. Bw. Walter alisema watoto walioweza
kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa msaada wa
shirika lake ni 40 na watoto 30
wameshindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wazazi
kutokuwa na uwezo wa kuwasafirisha watoto hao, pia changamoto ya
wananchi kuwa na imani potofu ya kuwa watoto hao wamerogwa
Huduma
hiyo inatolewa mkoani Kagera na shirika la Friends of Children with
Cancer Tanzania wakishirikiana na Madaktari wataalam wa upasuaji huo
kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando pia kutoka katika kitengo cha
Muhimbili Orthopaedic Instutite (MOI) kilichopo Hospitali ya Rufaa ya
Taifa Muhimbili.
Daktari Gerald D. Mayaya kutoka idara ya upasuaji Hospitali ya Rufaa
Bugando akielezea chanzo cha tatizo la ugonjwa wa kichwa kujaa maji na
mgongo wazi alisema kuwa ni mishipa ya kusafirisha maji kichwani kuziba
na kichwa huanza kuvimba ambapo kuna watoto huzaliwa na ugonjwa huo pia
wengine upatwa na ugonjwa huo
wakiwa tayari wamezaliwa na watu wazima pia hupatwa na ugojwa huo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. John Mongella baada ya kuzindua huduma hiyo
na kutembelea wodi ya watoto wenye tatizo la vichwa kujaa maji na mgongo
wazi alisema amejifunza mambo mengi maana mwanzo alijua kuwa ugonjwa
huo kwa watoto huzaliwa nao kumbe hata mara baada ya kuzaliwa au mtu
mzima anaweza kupatwa na ugonjwa huo.
Mhe
Mongella alitoa wito elimu kutolewa kwa wingi ili wananchi waweze kujua
kuwa ugonjwa huo unatibika ili wazazi na walezi waweze kuwaleta watoto
wenye tatizo hospitali ili wakatibiwe. Pia aliwashukuru Shirika la
FOCCTZ kwa kuzindua huduma hiyo ambayo aliita huduma takatifu kwani
inaokoa maisha ya watoto walio wengi.
Wito, Mhe. Mongella alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuweza
kushirikiana na shirika hilo ili kuchagia huduma hiyo kuokoa maisha ya
watoto. Pia alitoa wito kwa Wanahabari wa mkoa wa Kagera na Tanzania
kwaujumla kuelimisha jamii juu ya tatizo hilo ili liweze kupunguzwa kwa
kiasi kikubwa.
Naye Vaileth John Makula (32) mzazi wa Gib Philimoni kutoka Wilaya ya
Karagwe alilishukuru Shirika la FOCCTZ kuleta huduma hiyo Kagera maana
anasema kuwa
mwanae Gib alizaliwa katika hali ya kawaida na baada ya miezi minne
tatizo la kuvimba kichwa lilianza na alimpeleka mtoto wake katika
hospitali teule ya Wilaya Nyakahanga alikoambiwa ampeleke Bugando
ambako hakumpeleka kwa kukosa nauli. Mama Gib alishukuru na alisema ana
imani na madaktari hao kuwa watamponya mwanae Gib.
Madhara ya ugonjwa wa kichwa kujaa maji na mgongo wazi unaweza
kusababisha upofu wa macho, mtoto kutojiweza kabisa kutumia muda wote
akiwa amelala tu, pia huathiri ubongo, na wakati mwingine husababisha
vifo kwa watoto.
Kwa takwimu alizotoa Bw. Walter alisema kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa
duniani watoto 2 huzaliwa na tatizo la kichwa kujaa maji, kwa nchi ya
Tanzania watoto wote wanaozaliwa kwa mwaka watoto 4580 huzaliwa au
hupatwa na ugonjwa huo ambapo kila watoto 1000 wanaozaliwa watoto 3
huwa na
tatizo hilo.
Mganga Mfawidhi wa Haspitalia ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Dk. Juma
Nyakina aliwashukuru shirika la FOCCTZ na liwahakikishia kuwa hospitali
yake ipo tayari kwa kuwawekea mazingira mazuri wataalamu hao na kuandaa
vitendanishi ili waweze kuifanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa pia
alisema wataalam wa hospitali hiyo wapo tayari kujifunza na kupata ujuzi
huo.
0 comments :
Post a Comment