Mwenyekiti
wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda
wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari
Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa
mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo.
Viongozi wapya wa SPC wakiwa meza kuu.
Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang’anyi akizungumza baada ya uchaguzi, kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Stella Ibengwe.
Baadhi ya viongozi wa SPC wakiwa katika picha ya pamoja. Kadama Malunde Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga
…………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa
wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC) jana Julai 23, 2015 kimefanya
Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi
cha miaka mitatu mfululizo ambapo mwanahabari, Kadama Malunde
amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi
wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila
alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea
wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.
Kadama Malunde ni mwandishi wa
habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na Mkurugenzi wa Malunde1 blog
ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania
Bloggers Network, TBN).
Nkulila aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa
ni Stephen Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa
Makamu Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella
Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo, kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika klabu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.
Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku wakizingatia maadili ya wanahabari
0 comments :
Post a Comment