Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na
wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Tabora wakati alipokuwa
katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa
Tabora Mhe.Ludovick Mwananzila na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe.Suleiman
Kumchaya.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora
wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Kulia ni Mganga
Mkuu wa mkoa wa Tabora.IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na
Maafisa, wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa na Mganga Mkuu
wa Hospitali ya Polisi Dkt.Nyanda wakitoka kukagua Wodi ya wazazi
katika Zahanati ya Polisi Tabora baada ya kuizindua wakati alipokuwa
katika ziara ya kikazi katika mkoa huo..IGP pia alitumia ziara hiyo
kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiweka jiwe la
msingi katika jengo la Kikosi cha usalama barabarani mkoani Tabora
wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo pia
alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa
huo.Kulia ni Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Kamishna msaidizi
wa Polisi, Juma Bwire.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikagua ujenzi
unaoendelea wa Kituo cha Polisi na Makazi ya Askari Wilayani Ikungi
mkoani Singida wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa
huo.Katikati ni ni kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi
wa Polisi Thobias Sedoyeka na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ikungi.
Kamanda wa Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi
mwandamizi wa Polisi, Richard Malika akimtembeza Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu kuangalia ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani
Lushoto mkoani Tanga wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa
huo.
0 comments :
Post a Comment