William Malecela, maarufu kama Lemutuz Nation au "King of All Bongo
Social Networks" kama anavyofahamika katika mitandao mbalimbali ya
kijamii ameeleza sababu za yeye kutosomeshwa na baba yake mzazi.
Le Mutuz Nation ambaye ametumia muda mwingi kusoma na kuishi nchini
Marekani na Belgium, ameweka bayana katika kipindi cha Mlimanidotcom cha
Mlimani TV kuwa alijisomesha kwa kupitia fedha ambazo zilitokana na
kazi mbalimbali ambazo alikuwa akifanya kama vile udereva wa mabasi
makubwa huko jijini New York pamoja na kukaanga kuku.
Alipoulizwa kuhusu taarifa za yeye kujisomesha kupitia kuendesha malori
na kukaanga kuku, Le Mutuz alisema “Liko sawasawa, unajua ni la ajabu
Tanzania lakini si la ajabu nchi nyingine kwasababu mimi wakati nakua,
tulikuwa kwenye siasa ya ujamaa kwa hiyo mambo mengi yalikuwa yamebana
na mimi nilikuwa nataka ubaharia”
Alieleza kuwa sababu kuu ni kuwa yeye alitaka ubaharia lakini baba yake
hakutaka yeye asome masomo hayo katika ngazi ya chuo kikuu, Lakini pia
ameeleza kuwa baba yake ambaye ni Waziri mkuu wa zamani wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania hakumsomesha kwasababu kipindi yeye anakua ilikuwa
ni kipindi cha ujamaa na mambo mengi yalikuwa yamebana hivyo baba yake
asingeweza kumlipia kusoma nje ya nchi.
Pamoja na kueleza hayo, Lemutuz alizungumzia sababu za yeye kuliburuza
gazeti la Kiu mahakamani na pia kwanini anapenda kupiga picha na
wanawake na kuweka Instagram



0 comments :
Post a Comment