Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza Sept 12 badala ya Agosti 22 ili
kumpa Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake kuelekea mechi
ya Taifa Stars vs Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi
ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayozikutanisha Azam FC dhidi ya
Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22 badala ya Agosti 15.
Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa inafanyiwa marekebisho
kwa ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine mechi
sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya Oct 25
hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.
Wamiliki wa viwanja vyenye upungufu wmeandikiwa barua kutakiwa
kurekebisha upungufu katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa
kutumika kwa ajili ya PL na FDL.
Timu ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Nyerere uliopo
Mbulu mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu uliopo
kwenye uwanja huo urekebishwe kwanza.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)



0 comments :
Post a Comment