Live Dodoma: Polisi Watumia Mabomu Kuwatawanya Wafuasi wa Lowassa Waliokuwa Wakiandamana

Saturday, July 11, 2015

Nkupamah blog

Wapambe wa Mbunge  wa Monduli Edward Lowassa  hivi sasa wanafanya maandamano makubwa nje ya ofisi za CCM hapa makao makuu ya CCM wakipinga Mbunge huyo kuchujwa katika tano bora.

Wapambe hao wanaimba nyimbo mbalimbali za kukiponda chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa chama hicho sio cha kindugu na  pia sio cha kifalme.

Kwa namna nyingine  hali si shwari hapa mkoani Dodoma ambapo sintofahamu imetawala kuhusiana na Edward Lowassa kukatwa.

Bado haijulikana nini hatma ya kikao kinachoendelea hivi sasa kwa kuwa wa wajumbe wengi wanapinga Lowassa kuchujwa.
Biashara zimesimama,makao makuu Dodoma.
Baadhi ya wapambe wa Lowassa wakipinga Kamati kuu kumchuja Lowassa.
Barabara zafungwa Polisi watanda kila kona kudhibiti usalama dhidi ya waandamanaji.
Wapambe wa Loawssa wakipinga kukatwa tano bora.
  Nkupamah blog
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment