@nkupamah blog
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Zanzibar Dr. Jidawi akizungumza na Madaktari Diaspora kutoka Washington
walipofika Afisini kwake kwa kujutambulisha ujio wao Zanzibar walioletwa
na Jumuiya ya Watanzania Washington wakiwa chini ya uenyeji wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora Zanzibar na Benki ya Watu wa Zanzibar
(PBZ),wakiwa Zanzibar wametoa huduma ya kucheki waginjwa wa Kisukari na
Meno na kutoa Elimu ya Afya Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa
Zanzibar.
Picha zote na OthmanMapara.Blog. Zanzinews.Com.
Katibu Mkuu Dr Jidawi
akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Madaktari hao walipofika
Afisini kwake wakiwa na Ujumbe wa Watu 17 wakiwemo Madaktari wa Saratani
ya Matiti kwa Kina mama, Kisukari na Meno.
Madktari wa Diaspora kutoka Washington wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar walipofika Afisin kwake
Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu
Mhe Salum Maulid Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Diaspora
Zanzibar Ndg Adila Hilal Vuai wakiwa na wenyeji wao wakifuatilia
maongezi na Dr Jidawi walipofika kuwatambulisha madaktari hao. kupitia
Jumuiya ya Watanzania Washington.
Mkuu wa Ujumbe huo,Rais wa
Jumuiya ya Wanawake (Africa Womens Cancer Awareness Assciation) Dr Ify
Anne Nwabukwu akitowa shukrani kwa ushirikiano waliopata wakiwa Zanzibar
katika kufanikisha malengo ya kutowa huduma kwa Jamii ya Tiba ya
Saratani ya Matiti na Elimu ya vitendo kuhusiana na Viashiria vya
Saratani ya Matiti kwa Wanafunzo wa Chuo cha Elimu ya Afya Zanzibar.
Mkuu wa Ujumbe huo Rais wa

Daktari wa Meno akuzungumza
wakati wa mkutano huo na Katibu Mkuu Wizaya ya Afya Zanzibar walipofika
Afisini kwake kujitambulisha.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Saleh Mohammed Jidawi akipokea msaada wa Dawa
za Binaadamu kutoka kwa Daktari Jummy Amuwo kwa niaba ya Madaktari wa Dispora kutoka Washington wakiwa Zanzibar mualiko wa Jumuiya ya Watanzania Washingto,
akishuhudia Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe Salum Maulid, makabidhiano hayo yamefanyika katika Afisi za Wizara ya Afya Zanzibar

Rais wa Jumuiya ya Watanzania
Washington Ndg Iddi akiungezani na Katibu Mkuu Afisi ya Rais Ikulu Mhe
Salum Maulid baada ya makabidhiano ya madawa ya Binaadamu yaliotolewa na
Madaktari Diaspora Washington. hafla hiyo imefanyika Wizara ya Afya
Zanzibar.
Wakipongezani kwa ushirikiano waliouonesha kwa mapokezi waliopata wakipongezana baada ya hafla hiyo.
Madaktari Diaspora wakiwa katika
picha ya pamoja na wenyeji wao Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
Diaspora Zanzibar nje ya Jengo Wizara ya Afya Zanzibar baada ya hafla ya
kukabidhi dawa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dr Jidawi.
0 comments :
Post a Comment