- Written by Nkupamah log
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Ndugu Sabetha Mwambenja mara
baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Nyerere.
Maonesho hayo yalifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete
tarehe 3.7.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Ndugu Jacqueline Maleko mara
baada ya kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya Sabasaba
kwenye Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam tarehe 3.7.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Biashara wa TANTRADE, Ndugu Edwin Rutageruka wakati alipowasili kwenye
viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere kuhudhuria sherehe za
ufunguzi wa maonesho hayo uliofanya na Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya
Kikwete tarehe 3.5.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Anna Mkapa kutembelea
banda la Taasisi yake ya Fursa Sawa kwa wote (EOTF) mara baada ya
Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Kikwete kufungua rasmi maonesho hayo tarehe
3.7.2015.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiambatana na mwenyeji wake Mama Anna Mkapa
wakiangalia bidhaa mbalimbali za akina mama wajasiriamali kutoka mikoa
ya hapa nchini. Akina mama hao wanaratibiwa na Taasisi ya Fursa Sawa kwa
Wote inayoongozwa na Mama Anna Mkapa.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma
Kikwete akiwa na Mama Anna Mkapa wakifurahia bidhaa za vikapu
zilizotengenezwa na akina mama wajasiriamali kutoka mkoani Singida
kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayofanyika Dar es Salaam
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo ya bidhaa mbalimbali za asili
wakati alipotembelea banda la Fursa Sawa Kwa Wote kwenye Maonesho ya
Sabasaba tarehe 3.7.2015. Kulia kwa Mama Salma ni Mama Anna Mkapa
akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema.


0 comments :
Post a Comment