- Written by Nkupamah blog
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiongeza na washiriki katika tukio
la kuchangia mfuko kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa
saratani ambapo alisema kuwa wamiliki wa vyombo vya habari hawana budi
kuwajali wanahabari na kuwapatia huduma muhimu ikiwemo Mikataba ya Kazi
pamoja na Bima za matibabu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na
uadilifu, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. kulia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick na Kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Mkuu wa
Mkoa Dar es Salaam
Said Meck Sadick akiongeza na washiriki katika tukio
la kuchangia mfuko kwa ajili wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa
saratani ambapo aliipongeza kamati iliyoratibu shughuli hiyo kwa manufaa
ya waandishi wa habari na kuwataka kuukuza umoja huo kwa manufaa ya
wanahabari na umuhimu wa wanahabari katika jamii ya Kitanzania na
Duniani kwa ujumla.Kulia ni Mwenyekiti wa Kampeni hiyo iliyolenga kupata
fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu Bw.
Benjamin Thompson.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akimkabidhi Mwenyekiti
wa kampeni hiyo Bw. Benjamin Thompson fedha zilizochangwa na Maafisa
Habari wa Taasisi za Serikali kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari
wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, wakati wa mkutano uliofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul
Makonda.
Mkuu wa
Mkoa Dar es Salaam Said Meck Sadick akiosha gari kwa ajili ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa
saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.
Kiongozi
wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe akiosha gari kwa ajili ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa
saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiosha gari kwa ajili
ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu
hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akiosha gari kwa ajili ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa
saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa
Mkoa Dar es Salaam Said Meck Sadick akisalimia na Kiongozi wa Chama cha
ACT-Wazalendo Zitto Zubeir Kabwe walipokutana katika kampeni ya kuosha
magari ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika
viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanahabari na Maafisa Habari wa Taasisi za Serikali wakiwa katika picha ya pamoja katika kampeni ya kuosha magari ya wanahabari wanaougua magonjwa sugu hasa saratani, leo katika viwanja wa Leaders Jijini Dar es Salaa


0 comments :
Post a Comment