- Written by Nkupamah blog
John Bocco akishangila baada ya kuipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju
wa penati .
Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The
Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017
nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.
Stars
ambayo leo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la
kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji
Uganda.
Mpaka
dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 – 0
Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi
mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.
Dakika
ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo
la hatari.
Mara
baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa
Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa
mchezaji Kizito Hezron.
Mashabiki.
Mpaka
dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 – 1 Tanzania. Kwa matokeo
hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 – 1 na sasa
watakutana na Sudan.
Mara
baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema
anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri
timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja
iliyopatikana.
Mkwasa
amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda
mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko
yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa
muda mrefu ili kujenga timu bora.
Rashid Mandawa akimtoka Hassani Maswa.
Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.
Taifa
Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub,
Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla
John Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.
The
Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa,
Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik,
Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.
Kikosi cha Taifa Stars.


0 comments :
Post a Comment