Mtoto atekwa, abakwa hadi kupoteza maisha

Tuesday, July 7, 2015

  Nkupamah blog

Mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la Ester Banzi, mkazi wa Tabata Msimbazi, jijini Dar es Salaam, ametekwa na kubakwa hadi kupoteza maisha baada ya mtu asiyefahamika kufanya kitendo hicho na kutokomea sehemu isyojulikana.
 
Inadaiwa kuwa siku ya tukio mtoto huyo alikutwa amefariki baada ya kuingiliwa kimwili na mwanaume ambaye inadaiwa kuwa alimteka kwanza kabla ya kufanya kitendo.
 
Kwa mujibu mama mdogo wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Watende Hamis, amesema kuwa siku ya tukio mama wa marehemu (Rebeka) alimtuma Ester, dukani kununua unga na kudai kuwa  sio mara ya kwanza kwa mtoto huyo kutumwa dukani.
 
Inadaiwa kuwa muda ulizidi kwenda bila mtoto huyo kurudi kwani duka halikuwa mbali na nyumbani, ikabidi wamfuatilie kwa watoto wengine ambao huwa akicheza nao lakini hawakumpata na watoto hao walidai kuwa walimuona na mfuko wa rambo akiwa ameongozana na baba mmoja.

Amedai kuwa waliendelea na juhudi za kumtafuta na kumtaarifu baba mzazi wa mtoto huyo ambaye alienda kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi Tabata Shule, na kudai kuwa ndani ya masaa matatu baba wa mtoto huyo aliwapigia simu kuwa mtoto ameokotwa huku mwili ukionesha kuwa alibakwa na kuharibiwa vibaya.
 
Kwa mujibu wa majirani wamedai kuwa walisikia sauti ya mtoto akiomba msaada na ndipo wakaangalia eneo hilo na kumuona mtoto huyo na baada ya kumchunguza wakagundua kuwa amebakwa kwani nguo yake ya ndani ilikuwa pembeni.
Nkupamah blog
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment