Tuesday, July 7, 2015
Nkupamah blog
Diamond Platnumz amesema kuwa ameshafanya collabo na wasanii A-list
karibu wote wanaofanya vizuri Afrika, lakini hakuna hata mmoja ambaye
amewahi kumlipa wala wao kumlipa kwaajili ya collabo hizo.
“Nimefanya collabo na wasanii tofauti tofauti, karibuni A-list wote ya wanaofanya vizuri Afrika nimeshafanya nao.” Alisema kupitia XXL ya Clouds Fm.
Ameongeza kuwa mwanzoni haikuwa rahisi kufanya nao kutokana na kwamba wengi walikuwa hawamfahamu tofauti na ilivyo sasa.
“Kiukweli sijawahi kufanya malipo ya mtu yoyote kufanya naye
nyimbo. Mwanzoni wakati naanza kufanya ilikuwa kidogo tabu kwasababu mtu
alikuwa hajafahamu anafanya nyimbo na nani, lakini sasa hivi wanafahamu
kwamba…nikifanya nyimbo na Diamond, East Afrika mimi kwangu inakuwa
kiurahisi nyimbo yangu, na upande wangu mimi inakuwa ni rahisi kwa West,
kwahiyo tukichanganya inakuwa rahisi zaidi.
"Kwahiyo hakuna mtu ambaye
nimeshawahi kumlipa wala yeye mimi kunilipa hii ni uongo sijawahi
kufanya hivyo.”
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment