Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bw.
Nehemia Mchechu. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa Mkurugenzi huyo
Mbezi Beach jijini Dar es Salaam julai 23, 2015 kumpa pole kufuatia
kifo cha Baba yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi.
Marehemu atasafirishwa kuelekea
Muheza, Tanga kwa ajili ya Mazishi. Mazishi yatafanyika Kijiji cha
Enzi, Muheza – Tanga siku ya Jumamosi tarehe 25/07/2015.
PICHA ZOTE NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Marehemu John
Edward Mchechu ambaye ni baba wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa(NHC) Bw. Nehemia Mchechu. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa
Mkurugenzi huyo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam julai 23, 2015 kumpa
pole kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete
akiifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu Mbezi beach jijini
Dar es Salaam julai 23, 2015. (wapili kushoto) mtoto wa Marehemu ambaye
ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu.
Familia ya marehemu John Edward Mchechu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete
akiondoka mara baada ya kuifariji familia ya marehemu John Edward
Mchechu (katika) mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC
Bwana Nehemia Mchechu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete
akiagana viongozi mara baada ya kuifariji familia ya marehemu John
Edward Mchechu (katika) mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa
NHC Bwana Nehemia Mchech.
Waombolezaji.


0 comments :
Post a Comment