Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Kwa ufupi
Baada ya Mahakama kufuta shtaka hilo la kwanza, sasa Ponda atatakiwa kujitetea mashtaka mawili yaliyobaki.By Lilian Lucas
Morogoro. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, jana ilimfutia
shtaka moja kati ya matatu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Baada ya Mahakama kufuta shtaka hilo la kwanza, sasa Ponda atatakiwa kujitetea mashtaka mawili yaliyobaki.
Mahakama hiyo iliridhika na upande wa mashtaka uliowasilisha ushahidi, hivyo Ponda atajibu shtaka la pili na tatu.
Akitoa uamuzi mdogo kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au la, Hakimu Mary Moyo alisema Ponda ana mashtaka mawili ya kujibu.
Mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Ponda baada ya kufikishwa mahakamani
hapo Agosti 18, mwaka 2013 ni pamoja na kutoa kauli za kuwataka Waislamu
kutokubali kuundwa kwa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwa vile
ziko chini ya Bakwata, ambao ni vibaraka wa CCM na Serikali.
Hakimu Moyo alisema shtaka analotakiwa kujitetea ni lile alilotenda
Uwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, ambapo anadaiwa kuituhumu
Serikali kupeleka wanajeshi Mtwara kuzima vurugu za kupinga gesi kuletwa
Dar es Salaam, lakini wananchi wa huko wakaishia kuuawa, kubakwa na
kuteswa kwa vile asilimia 90 ya wakazi wake ni waislamu.
Ilidaiwa pia kuwa Ponda aliituhumu Serikali kutopeleka polisi Loliondo
baada ya wananchi kupinga Mwarabu kupewa kipande cha ardhi ya uwindaji
na hiyo ni kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni Wakristo.
Katika shtaka la tatu, Ponda anadaiwa kuwa kauli alizotoa kuhusu
wanajeshi walioua, kubaka na kutesa wananchi na madai kuwa asilimia 90
ya wananchi wa Mtwara ni Waislamu, zililenga kuumiza dini ya watu
wengine, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha Sheria Namba 390 na
Kanuni ya Adhabu Namba 35 cha mwaka 2002.
Akifafanua, Hakimu Moyo alisema kuwa katika kosa la kwanza, mahakama
hiyo imeona Ponda hana kesi ya kujibu kwa vile tayari shtaka hilo
lilishatolewa uamuzi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kwamba
mahakama ya chini haina uwezo wa kupinga.
Baada ya hakimu huyo kutoa uamuzi huo, upande wa utetezi ukiongozwa na
Wakili Juma Nassoro uliridhika na uamuzi huo na kwamba wako tayari
kuleta mashahidi katika kesi hiyo.
Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili Sunday Hyera, uliomba kupangiwa
tarehe nyingine ya kuwasilisha ushahidi wa upande wa utetezi kwa vile
Wakili Kiongozi, Bernard Kongola alishindwa kufika mahakamani kwa sababu
zilizo nje ya uwezo. Kesi hiyo itaendelea tena Agosti 7.
Credet:mwananchi tz


0 comments :
Post a Comment