Monday, July 6, 2015
Nkupamah blog
RAIS
Jakaya Kikwete, amewataka viongozi wa dini nchini kutowapa mwanya
wanasiasa wenye dhamira ovu ya kuwafarakanisha Watanzania bali waendelee
kukemea matumizi mabaya ya fedha, rushwa na hujuma katika Uchaguzi Mkuu
hasa kipindi hiki.
Alisema
ipo haja ya viongozi hao kuendelea kuwakemea wanasiasa wanaopenda
madaraka kwa gharama yoyote wakitumia fedha kununua ushindi au ubaguzi
wa rangi, kabila, dini, kuwabagua wapinzani wao na kujijenga zaidi
kisiasa.
Rais
Kikwete aliyasema hayo jana katika Maadhimisho ya Miaka 125 ya Injili
katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), yaliyofanyika katika Viwanja vya Mbuyukenda,
mkoani Tanga.
Aliwaomba
viongozi wa dini na wananchi, wasiwasikilize wanasiasa wenye dhamira
ovu wala kuwaendekeza kwani mchezo wao ni mauti ya Watanzania hivyo
wawakatalie kwa macho makavu.
Alisema
si vyema kukaa kimya dhidi ya watu wanaokiuka maadili na kuchochea
mifarakano katika Taifa kwani watu hao si wema bali wataifikisha nchi
pabaya hivyo wasiruhusiwe kuchezea dini zetu ambazo ni mhimili muhimu wa
amani yetu tofauti na ukabila.
"Tusikubali
kumchukiza Mungu akatukasirikia na kutuadhibu kwa jambo ambalo liko
ndani ya uwezo wetu kulizuia lisitokee, mambo yakiharibika hatuwezi
kumlaumu mtu mwingine yeyote bali sisi wenyewe.
"Katu
hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu bali itakuwa ni makosa yetu
wenyewe, nawaomba viongozi wa dini mlisaidie Taifa letu, limeni mraba
wenu vizuri nasi tulime wetu, msiwape nafasi viongozi wa siasa na hata
wa dini kutumia majukwaa ya dini kuendeleza maslahi yao ya kisiasa hasa
kupandikiza chuki katika jamii," alisema.
Rais
Kikwete aliongeza kuwa, Serikali inawategemea viongozi wa dini wasiwe
sehemu ya makundi ya wagombea au vyama vya siasa bali wanapaswa kuwa
pande zote ili waweze kufanya vizuri kazi yao ya kuliponya Taifa kama
kutatokea matatizo.
Aliongeza
kuwa, Serikali haitegemei viongozi wa dini wawapangie waumini wao vyama
au viongozi wa kuwachagua bali wawahimize na kuwakumbusha waweze
kutumia haki na wajibu wao vizuri.
"Muwakumbushe
mambo muhimu matatu, kwanza kujiandikisha, pili, kujitokeza kwenda
kupiga kura, tatu kuchagua viongozi wazuri wasio waovu, wasiofanana na
uovu na kuukaribia uovu, watakaosukuma mbele gurudumu la maendeleo na
kujali maslahi mapana ya jamii husika na nchi yetu," alisema Rais Kikwete.
Aliwaomba
waendelee kuiombea Tanzania iendelee kuwa ya amani na utulivu ili watu
wake wadumishe upendo na mshikamano miongoni mwao na kuombea Uchaguzi
Mkuu ujao uwe salama ili Taifa lipate viongozi wazuri, liendelee kuwa
tulivu kabla, baada ya uchaguzi.
Alisema
historia inaonesha kuwa, katika nchi nyingi za Afrika wanasiasa hutumia
kupindi cha uchaguzi kufanya maasi hivyo uadilifu na tahadhari kubwa
inahitajika.
Kwa
upande wake, Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,
Dkt. Stephen Munga, alisema ili Taifa liweze kuvuka kipindi cha uchaguzi
salama, Uchaguzi Mkuu ufuate misingi yote iliyowekwa na Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC), ili kuwapa uhuru wananchi waweze kuchagua viongozi
wanaowataka.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment