Baadhi
ya wadau wa Sekta binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakifuatilia
ajenda wakati wa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) juu ya
kuleta maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini.
Na Benedict John-MAELEZO-Dar es salaam
Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) imeadhimia kuhusisha Sekta binafsi pamoja na
benki nchini ili kuongeza kasi ya usambazaji umeme Vijijini.
Hatua hiyo itasaidia kuleta maendeleo ya haraka na kufikisha umeme katika maeneo ya vijijini katika maeneo mengi hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava wakati akiongea katika
kikao kilichohusisha Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, sekta binafsi
pamoja na benki zilizopo nchini.
Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Wakala wa Nishati Vijijini , kasi ya upelekaji umeme vijijini hapa nchini imeogezeka.
“Baada
ya hiki chombo kuingia kazini kasi imeongezeka kwani kwa sasa wananchi
waliofungiwa umeme ni zaidi ya asilimia 24 na wakati ule namba ya uwepo
wa umeme vijijini ilikuwa asilimia 10 mwaka 2005 ambapo kwa sasa ni
karibu asilimia 40 na tunatarajia kuongeza kasi hii kadri tunavyozidi
kupata vyanzo vingi vya fedha kwani malengo yetu hapo baadaye ni kuweza
kufikia asilimia zaidi ya 70”, alisema Mhandisi Mwihava
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini, Dkt. Lutengano
Mwakahesya ameeleza kuwa kikao hicho kinalenga kufafanua namna gani
sekta binafsi zinavyoweza kupata faida kwa kuingia katika sekta ya
nishati pamoja na kushirikia katika kuleta maendeleo ya haraka katika
kufikisha umeme kwa asilimia 60 na zaidi.
Amesema
kuwa endapo umeme nchini utaenea katika maeneo ya vijijini utaweza
kuleta maendeleo makubwa hususani katika kuleta ajira kwa vijana na
kuibua miradi mbalimbali kupitia viwanda vidogo vidogo jambo ambalo
litapunguza tabia ya baadhi ya watu kukimbilia mijini katika kusaka
ajira.
“Maendeleo
makubwa yatapatikana iwapo umeme huu utafika vijijini, utasaidia kuleta
viwanda vido vidogo kama vile mashine za kukoboa ili ipatikane ajira
vijijini na watu waache kuhamia mjini nkutafuta maisha bora kwanbi umeme
huu utasaidia wawananchi kuibua miradi mizuri ya maendeleo”. Alisema
Mwakahesya.
Ameongeza
kuwa, watu wengi hawawezi kulipa shilingi 27,000 hivyo Bodi hiyo
inatazamia kuongea na benki za zilizopo nchini pamoja na sekta binafsi
ili kuweza kupata njia bora zaidi za kufikisha umeme katika maeneo hayo
ya vijijini kwa kuwapa mkopo ambao unaweza kulipwa pole pole kwa kutumia
kulipia bili za umeme.
Serikali
ilikamilisha mchakato wa uanzishwaji wa Taasisi ya Wakala wa Nishati
Vijijini mnamo mwaka 2005 ambapo mwaka 2007 hadi hivi sasa baada ya
Wakala kuingia kazini, kasi ya upelekaji ya umeme vijijini imekuwa
kubwa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa Sekta
binafsi pamoja na benki zilizopo nchini wakati wa kikao kilichofanyika
katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kati ya Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) juu ya kuleta maendeleo ya usambazaji wa umeme
vijijini .(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO).
0 comments :
Post a Comment