Wandishi wa Habari Wanawake
wametakiwa kujitokeza kugombania nafasi za Uongozi katika Chama cha
Wandishi wa Habari Zanzibar (Zanzibar Press Club) ili waweze kutoa
mchango wao katika kukiendeleza Chama hicho.
Hayo ameyasema Katibu wa Chama
cha Waandishi wa Habari Zanzibar Suzan Kunambi wakati akizungumza na
Mwandishi wa habari hii katika Ofisi ya Chma hicho Kijangwani Mjini
Zanzibar.
Amesema wanawake wanamchango
mkubwa katika kuimarisha maendeleo ndani ya Vyama na Jumuia za Kiraia
lakini wamekuwa hawajitokezi katika kugombania nafasi za uongozi na
kupoteza fursa hiyo muhimu kwao.
Aidha ameelezea lengo la la
kuanzishwa Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar ni kuwaunganisha
waandishi wa Habari pamoja ili waweze kuzitafutia ufumbuzi changamoto
zinzowakabili katika kazi zao za kila siku.
Amesema kuwa Chama hicho
kimefanikiwa kuwasaidia wanachama wake kwa kuwapatia mafunzo ya
muda mfupi ya uwandishi wa habari yakiwemo kuandika habari za
Biashara, Mazingira na habari za Kimitandao .
Hata hivyo amezitaja baadhi ya
changamoto zinazokabili chama hicho kuwa ni pamoja na ukosefu wa Fedha
na Ofisi ya kudumu ya kuendeshea shughuli zao na kuweza
kujitegemea.
Kunambi amewaomba waandishi wa
Habari wa Zanzibar kujitokeza kujiunga katika Chama hicho ili kiweze
kupata nguvu na kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuanzishwa
kwake.
0 comments :
Post a Comment