Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea maelezo kuhusu utekelezaji
wa majukumu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
kutoka kwa Ofisa wa HESLB Bi. Veneranda Malima katika maonesho ya vyuo
vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha na
HESLB).
Ofisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bw. Saleko
Mandara (kushoto) akimwelekeza namna ya kujaza fomu ya kurejesha mkopo
Bw. Suleiman Zidi Hisabu ambaye ni mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha
Abdulrahman Al-Sumait Zanzibar na mnufaika wa mkopo aliopewa na HESLB.
Bw. Hisabu alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha na HESLB).
Mkurugenzi
wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof.
Sylvia Temu akimkabidhi Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB) Bi. Veneranda Malima cheti cha ushiriki katika maonesho ya
vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ofisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Joyce Mgaya
(kulia) akijibu maswali ya Bi. Dorah Kusiri, mkazi wa jijini Dar es
Salaam kuhusu huduma za HESLB. Bi. Kusiri alitembelea banda la HESLB
katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini
Dar es Salaam.
Ofisa
wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bi. Joyce Mgaya
(kulia) akimwelekeza Bw. Sheha Semtawa (aliyekaa) namna ya kujaza fomu
ya kuomba mkopo kwa njia ya mtandao. Bw. Semtawa alitembelea banda la
alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mwisho wa kuwasilisha maombi ya
mkopo ni Julai 31, 2015. (Picha na HESLB).
0 comments :
Post a Comment