Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Zamaradi Kawawa
akimtambulisha (Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wa Diaspora, Rosemary Jairo, (Kulia).
Bi. Jairo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).(P.T)
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, kwa
kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade
Centre Un-Agency), inatarajia kuitisha kongamano kubwa la aina yake
likiwa na lengo la kuhamasisha ukuzaji wa biashara ndogo na za kati.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jioni jijini Dar, Mkurugenzi wa Idara ya
Watanzania waishio nchi za nje katika Wizara ya Mambo ya Nje (Diaspora),
Bi. Rosemary Jairo amesema, kongamano hilo litafanyika katika Hoteli ya
Serena jijini Dar, kuanzia Agosti 13 – 15 mwaka huu.
Alisema,
lengo kuu ni kuwahamasisha Watanzania waishio nje, kuwa na moyo wa
kujitolea katika uendelezaji na ukuzaji wa biashara ndogo na za kati
jambo ambalo kwa sasa linafanyika kwa kiwango na kasi duni. Pia, alisema
kongamano hilo litahusisha Wizara za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri
Mkuu.
Kikao
hicho kinatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kufungwa na Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Aliongeza, washiriki wa Diaspora katika kongamano hilo watapata fursa ya kufanya ziara visiwani Zanzibar kwa mwaliko maalum.
Habari / Picha: Na Denis Mtima / GPL.


0 comments :
Post a Comment