Maradhi ya Alzheimer huua seli za ubongo
Data zinasubiriwa kwa hamu kuhusu dawa inayotumainiwa kuponya ugonjwa wa udhoofu wa ubongo (Alzheimer) baadae leo .
Watafiti
watatangaza matokeo ya uchunguzi kuhusu matumizi ya dawa aina ya
solanezumab, ambayo wagonjwa na wanasayansi wanatuami inaweza kuwa tiba
ya kwanza ya kupunguza kasi ya kupungua kwa kazi ya ubongo
Dawa iliyopo kwa sasa inasaidi kupunguza dalili , lakini haisitishi kufa kwa seli za ubongo.
Dr Eric
Karran, kutokakituo cha utafiti wa maradhi hayo nchini Uingereza ,
anasema dawa hiyo inaweza kuhakikishwa kuwa na "uwezo mkubwa".BBC
Maradhi ya Alzheimer yanashambulia seli za ubongo
Maelezo ya uchunguzi kuhusu dawa ya solanezumab yatatolewa katika mkutano miji Washington.
Dawa hiyo
imekua matumaini makubwa ya malengo ya utafiti unaolenga seli za
protini ziitwazo amyloid ambazo humea kwenye ubongo mtu anapokuwa na
maradhi ya Alzheimer .
Inadhaniwa kuwa kuundwa kwa lundo la amyloid baina ya neva za seli kunasababisha kuharibik na baadae kufa kwa seli za ubongo.
Ugonjwa wa Alzheimer unawaathiri mamilioni ya watu duniani
Majaribio ya sawa ya maradhi hayo yanayowakumba mamilioni ya watu duniani yaligonga mwamba mwaka 2012.
Hata
hivyo, wakati kampuni ya Marekani ya Eli Lilly ilipoangalia kwa makini
data, ilibainika kuwa kuna ishara inaweza kufanya kazi kwa wagonjwa
wanaoanza kupata ugonjwa huo.


0 comments :
Post a Comment