Tuesday, July 28, 2015
@nkupamah blog
Kumekuwa na uvumi mkubwa juu ya shindano kubwa la TV Africa, Big Brother Africa (BBA) kutokufanyika mwaka huu na inadaiwa sababu ni ukosefu wa wadhamini wa shindano hilo.
Waandaaji
wa shindano hilo, Africa Magic na Endemol wamesema shindano hilo la BBA
2015 linaweza lisifanyike mwaka huu na hivyo kuahirishwa mpaka mwakani.
Manager
wa Multichoice Ghana, Anne Sackey amethibitisha uvumi wa taarifa hizo
kwa kusema kuwa wao Multichoice Ghana walipokea taarifa kutoka MNET kuwa
shindano la BBA mwaka huu halitofanyika kama ilivyozoeleka.
bba2
Anne
Sackey amesema kuwa MNET hawajatoa sababu za kwanini shidano hilo
halitofanyika mwaka huu lakini kwa upande wake anaamini kuahirishwa kwa
shindano hilo ni kutokana na ugumu wa kupata wadhamini kwani kuendesha
kipindi hicho hugharimu pesa nyingi sana.
@nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment