ULINGO WA
WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni
shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo
watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa
mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga
kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. Mafunzo hayo yamedhaminiwa
na UNWomen.
Mafunzo hayo
yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji
wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha
wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo
pale Student Center.
0 comments :
Post a Comment