Published in
Jamii
WATEJA
wapatao 157 wamekamatwa na Shirika la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa
Pwani kwa kosa la kuiba umeme na kuhujumu miumndombinu kinyume cha
sheria na taratibu na kupelekea
kulisababishia hasara shirika hili kiasi
cha shilingi milioni 178 kutokana upotevu wa umeme ulitumika bila ya
kulipiwa.
Kubainika
kwa wezi hao wa umeme kumetokana na kufanyika kwa operesheni kabambe
iliyofanywa na wakaguzi na maafisa mbali mbali kutoka kanda ya Dar es
Salaam na Pwani na kukuta watu hao wanaiba nishati ya umeme kinymemela
bila ya kufuata utaratibu.
Akizungumza
na waandishi habari kuhusiana na wizi huo Mhandisi mkuu wa kitengo cha
ukaguzi wa mita na mdhibiti wa mapato kanda ya Pwani na Dar es Salaam
Mrisho Sangiwa alisema kwamba kutokana na wizi huo kumefanya shirika
hilo kupoteza kiasi kikubwa cha makusanyo ya mapato yao kutokana na
vitendo vya wizi.
Sangiwa
aongeza kuwa Tanesco kanda ya Dar es Salaam na Pwani wameamua kulivalia
njuga suala hilo baada ya kugundua kuna baadi ya wateja wamekuwa
wakifanya ujanja wa kuhujumu miumbombinu yao pamoja na kuiba hali ambayo
inarudihs nyuma mipango waliyojiwekea katika kuboresha huduma ya
nishati ya umeme kwa wateja wao.
“Zoezi
hili tumeamua kuliendesha katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Pwani na
msako huu lengo ikiwa ni kuwabaini wale wote ambao wamekuwa na tabia ya
kuiba umeme na kuhujumu uchumi wan chi, hivyo kufanyika kw zoezi ii nin
aimani kubwa kutaweza kupunguza kasi ya wizi wa umeme,”alisema Sangiwa.
Sangiwa
alifafanua kwa sasa wateja ambao tayari wamewafanyia ukaguzi wa
kuziangalia mita zao wanazidi 4200 ambao kati ya hao 157 ndio
waliobainika wanaiba umeme kwa kijiunganishia kinymemela kitu ambacho ni
hatari kwa usalama wa maisha yao.
Naye
Afisa usalama wa Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba
akizungumzia kuhusina na mikakati waliyojiwekea katika kudhibiti wezi
hao alisema kwamba wamejiwekea mikakati kabambe ya kufanya misako ya
mara kwa mara nyumba hadi nyumba ili kuweza kuwabaini watu wachache
ambao wanahujumu miundombinu ya Tanesco.
Afisa
huyo alisema kwamba baada ya kumamatwa kwa wezi hao wa umeme kuna baadhi
ya watu 26 tayari wameshafungulliwa mashitaka kwa kukutwa na makosa ya
jinai ya kuhujumu miundombinu ya Shirika kinyume cha sheri na kwamba
watachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hiyo.
Katika
hatua nyingine Afisa usalama huyo amewatahadharia wananchi wa Mkoa wa
Pwani na Taifa kwa ujumla kuwa makini na watu ambao wanajifanya ni
wafanyakazi halali wa tanesco kumbe ni vishoka kitu ambacho amedai ni
hatari .

0 comments :
Post a Comment