TANZIA: APOSTLE JOHN KOMANYA AFARIKI.


Marehemu Apostle John Komanya
Taarifa ambazo zimetufikia alfajiri ya leo na kisha kuthibitishwa
punde, zinaeleza kwamba Askofu Mkuu na mwanzilishi wa kanisa la
Cathedral of Joy (CoJ), Apostle John Komanya, amefariki dunia alfajiri
ya saa kumi kwenye hospitali ya HIndu Mandal, jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel John Kigeli,
ameieleza GK kwamba Apostle Komanya alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya
kisukari pamoja na typhoid, na kwamba siku za nyuma alikuwa amelazwa
Hospitali ya Muhimbili, ambapo alikuja kuruhusiwa baada ya kupata
ahueni.

Siku mbili nyuma ndipo alipozidiwa tena na hivyo kupelekwa Hospitali
ya Hindu Mandal, ambapo mauti yalimkuta hapo. Marehemu ameacha mke na
watoto 3 ambao wako nchini Marekani, sehemu ambayo pia alikuwa
akihudumu.

Kwa sasa ratiba za ibada ya kanisa la CoJ ambalo lipo Gogoni Kiluvya,
zimehamishiwa kwa dada wa marehemu, Makoka, ambapo ibada huanza saa
nne asubuhi.

GK itaendelea kukuletea taarifa mpya kwa kadri itakavyokuwa inazipata.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina la BWANA lihimidiwe.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment