- Written by Nkupamah blog
Afisa
Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akiwasikiliza
wateja waliotembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la
Wizara ya Fedha.
Afisa
Masoko Bi. Kilave Atenaka (Kushoto) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) wakiwa na nyuso
za furaha na Bi. Beatrice Ngoda katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya
Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya
Saba Saba katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya
banda la Wizara ya Fedha.
Afisa
Masoko Bi. Mary Minja (Kulia) wa Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya
Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha (UTT –PID) akimsikiliza mteja
aliyetembelea katika banda kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya
Kimataifa, Dar es Salaam yanayoendelea katika mabanda ya Saba Saba
katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ndani ya banda la
Wizara ya Fedha.
Taasisi
ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya Wizara ya Fedha
(UTT –PID) ipo kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es
Salaam yananoendelea katika mabanda ya Saba Saba katika Viwanja vya
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Banda la
UTT PID lipo jirani na kuingia katika Banda la Wizara ya Fedha upande wa
kulia… karibuni sana wananchi mnaombwa kujitokeza kwa wingi mjipatie
huduma mbali mbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwemo huduma za
uuzwaji wa viwanja katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo vile vya mradi wa
katika Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundo Mbinu iliyochini ya
Wizara ya Fedha (UTT–PID) miji ya Chalinze na Bagamoyo mkoani Pwani.
Akielezea
Afisa Masoko Bi. Kilave Atenaka alisema kuwa kwa sasa wanaendesha
huduma ya uuzwaji wa Fomu kwa ajili ya Viwanja, pia wanatarajia kuanza
kuuza kwa umaa na taasisi mbali mbali miradi mipya ikiwemo wa Tundwi
Songai – Kigamboni jijini Dar es Salaam na ule wa Kingorwila, Morogoro.
Aidha Bi.
Kilave alitumia wito huo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi
ndani ya banda hilo kujipatia elimu mbali mbali zitolewazo na taasisi
hiyo hapa nchini.
Kwa sasa
UTT PID ni miongoni mwa taasisi zinazofanya vizuri katika utoaji huduma
za ushauri katika maeneo ya upembuaji yakinifu wa miradi mbali mbali,
uratibu wa fedha na huduma zinazohusian katika maandalizi ya mapendekezo
ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma
kuhusiana na maandalizi y a zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao
ni utoaji wa huduma fanisi za usimizi wa majengo yaliyochini ya
uangalizi thabiti wa taasisi.
0 comments :
Post a Comment