- Written by Nkupamah blog
Kaimu
Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa pili
kulia) akiwakabidhi watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa
Huruma, kilichopo eneo la Madale
Wazo Hill nje kidogo ya jiji la Dar es
Salaam
Kaimu
Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa
kwanza kulia walosimama) akizungumza na watoto wa Kituo cha watoto
yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo
ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya
saruji. Wengine ni wafanyakazi wa TTCL na kituo hicho
Kaimu
Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha (wa pili
kulia walosimama) akizungumza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha
Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam kabla ya kuwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.
Baadhi ya
wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiimba na
kucheza na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma,
wapopokuwa wakiwakabidhi msaada wa mifuko 70 ya saruji.
Baadhi ya
wafanyakazi na maofisa wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakipiga
picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma,
pamoja na wasimamizi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada wa
mifuko 70 ya saruji
Saruji
mifuko 70 ikishushwa kwenye gari mara baada ya kukabidhiwa watoto wa
Kituo cha watoto yatima cha Mama wa Huruma na kampuni ya TTCL.
KAMPUNI ya
Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaada wa mifuko ya saruji kwa kituo cha
watoto yatima cha Mama wa Huruma, kilichopo eneo la Madale Wazo Hill nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mifuko hiyo 70 ya saruji imekabidhiwa juzi katika kituo hicho na Kaimu Mkuu wa Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bw. David Dirisha kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.
Akikabidhi msaada huo, Bw. Dirisha alisema kampuni imetoa msaada huo ili kusaidia ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wale wenye mahitaji maalum. Alisema msaada huo waliokabidhi utasaidia kituo hicho kuwa na majengo yake yenyewe kwani kwa sasa wamejihifadhi katika eneo dogo na ambalo sio rafiki sana kwa watoto.
Kwa upande wake, Mtawa anayewalea watoto hao, Sr. Christina akipokea msaada huo alisema, anaishukuru kampuni ya TTCL kwa msaada huo; kwani umekuwa chachu ya kuamini kuwa na wao watakuwa na majengo yao na wataweza kusaidia watoto wengi zaidi.
Aidha ametoa wito kwa wadau wengine watakao guswa zikiwemo kampuni na taasisi mbalimbali kusaidia kituo hicho ili kiweze kukamilisha kwa wakati ujenzi wa majengo yake na hatimaye kuhudumia watoto wengi zaidi huku kukiwa na usalama wa kutosha.
Hii ni mara ya pili kwa TTCL kukichangia kituo hicho mifuko ya saruji kwani mwaka jana pia ilitoa msaada wa saruji kwa kituo hicho cha watoto yatima cha Mama wa Huruma ambacho kwa sasa kina idadi ya watoto 56 ambapo wavulana ni 26 na wasichana 30.

0 comments :
Post a Comment