Utiaji saini waraka wa maadili ya uchaguzi kwa vyama vya siasa

Naibu katibu Mkuu wa Chadema tawi la zanzibar Salum Mwalim akielezea maswala mbalimbali kuhusiana na hali ya Usalama kuelekea katika Uchaguzi mkuu katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palace Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa vyama vya Siasa waliohudhuria katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palace Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya ZEC Nassor Khamis Mohammed akifafanua baadhi ya mambo katika hafla ya utiaji Saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palace Zanzibar. 
Naibu Katibu Mkuu wa ATC - Wazalendo Juma Said Sanani akitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palace Zanzibar
Mwakilishi wa CCM Hafidh Ali akitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palace Zanzibar. 
Naibu katibu Mkuu wa Chadema tawi la zanzibar Salum Mwalimakitia saini waraka wa maadili ya Uchaguzi kwa vyama vya Siasa Grand Palace Zanzibar. 


Na Faki Mjaka-Maelezo
Hatimaye Vyama vya Siasa nchini vimesaini Waraka wa Maadili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 baada ya mjadala mkali.

Utiaji wa saini umefanyika leo katika ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace mjini Zanzibar baina ya Vyama vya Siasa, Tume ya Uchaguzi Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar huku wakishuhudiwa na Wawakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango na Maendeleo UNDP.

Mjadala huo ulitokana na kukosekana kwa Wadau muhimu katika Waraka huo ambao ni Chama cha Mapinduzi CCM na Jeshi la Polisi.

Hata hivyo Mwakilishi wa CCM baada ya muda kupita alifanikiwa kuja katika Mkutano huo na hivyo kupelekea Wadau wa vyama vingine kuridhia kusaini Waraka huo.

Akielezea umuhimu wa Maadili hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili hayo Nassor Khamis Mohamed amesema ni kuhakikisha uchaguzi Mkuu unaokuja unafanyika katika mazingira ya amani na utulivu kwa kuzingatia uhuru na haki ya ushiriki wa makundi yote ya kijamii kwa vigezo vya kimataifa.

Aidha amesema Waraka huo utaanza kutumika baada ya uteuzi wa Wagombea katika vyama vyao na ukomo wa matumizi yake utakuwa ni mwezi mmoja baada ya uchaguzi Mkuu kufanyika.

Miongoni mwa vipengele vya maadili hayo ni kupinga matumizi ya Siasa ya aina yoyote ya kutumia Viongozi, Wanachama, Wafuasi kwa malengo ya kufanya hujuma katika harakati za kisiasa.

Aidha maadili hayo yanakataza Vikundi vya ulinzi vya vyama kutumiwa kwa malengo ya kuchochea fujo na kuvuruga mani wakati wa Kampeni na Uchaguzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salum Jecha amewatoa wasiwasi Wawakilishi wa Vyama na kusema kuwa Maadili hayo yatatumika ipasavyo ili kuwa na Uchaguzi wa Amani na utulivu.

“Wajumbe msiwe na wasiwasi na Tume na tutafanya kila liwezekanalo ili tuwe na uchaguzi huru na wahaki” Alisema Mwenyekiti Jecha.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Issa Ibrahim Mahmoud amesema jukumu la Serikali ni kuhakikisha amani na utulivu inakuwepo muda wote na kwamba wataendelea kushirikiana na Tume ili kutimiza lengo hilo.

Kwa upande wao Wajumbe wa Vyama vya siasa wameitaka Kamati hiyo kulitafuta Jeshi la Polisi ili kusaini waraka huo ambao ni muhimu katika kustawisha hali ya amani na utulivu.

Itakumbukwa kuwa Katika Waraka huo Jeshi la Polisi ni Mdau muhimu na wamekuwa wakishiriki matayarisho ya Waraka huo katika kila kipengele lakini leo hawakufika kutia saini bila ya taarifa yoyote.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeahidi kulitafuta Jeshi la Polisi ili kufahamu zaidi dharura yao iliyopelekea kushindwa kutuma Mwakilishi wa kusaini Waraka huo wa Maadili ya Uchaguzi ya Vyama vya Siasa 2015.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment