Saturday, July 11, 2015
Nkupamah blog
Mmoja wa viongozi wa mapinduzi yaliyozimwa nchini Burundi hivi karibuni ya kutaka kumwondosha madarakani Rais Pierre Nkurunziza, amesema mikakati mingine inaendelea kupangwa ili kumng’oa kiongozi huyo madarakani.
Waasi hao wameyaambia mashirika ya habari ya
kimataifa kuwa wamekuwa wakiwapa mafunzo polisi na askari kwa ajili ya
jaribio lingine la kumwondoa Rais Nkurunziza.
Wamesisitiza kuwa azma ya kumwondosha kiongozi
huyo madarakani bado ipo palepale na kwamba kinachoendelea kufanyika
sasa ni kuratibu mikakati ya kufanikisha mpango huo.
“ Wakati ule (Mei) tulishindwa kumwondosha Rais Nkurunziza madarakani”, alisema Jenerali Leonard Ngendakumana wakati akihojiwa na shirika la habari la Reuters na kuongeza kuwa; “ mkakati wetu bado uko palepale,”.
“ Wakati ule (Mei) tulishindwa kumwondosha Rais Nkurunziza madarakani”, alisema Jenerali Leonard Ngendakumana wakati akihojiwa na shirika la habari la Reuters na kuongeza kuwa; “ mkakati wetu bado uko palepale,”.
Wapinzani hao wanampinga hatua ya Rais Nkurunziza
kuwania muhula mwingine wa tatu wa uongozi kwa maelezo kuwa kitendo
hicho kinakiuka katiba na kwenda kinyume na maridhiano ya Arusha
yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika hatua nyingine kuna ripoti kuwa, Rais
Pierre Nkurunziza wa Burundi ameashiria uwezekano wa kuahirishwa kwa
uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Shirika la Habari la China,Xinhua limemnukuu Rais Nkurunziza akitangaza hayo katika moja ya kampeni zake za uchaguzi huo.
Rais huyo amesikika akisema kuwa hatua hiyo
inakwenda sambamba na mapendekezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
iliyotaka kuahirishwa uchaguzi huo ili kupisha upatanishi.
Uchaguzi wa Rais nchini Burundi umepangwa
kufanyika Julai 15 lakini Jumuiya ya Afrika Mashariki imependekeza
kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo ili kumpa nafasi mpatanishi wa jumuiya
hiyo, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ya kuweza kuzungumza na
kuzipatanisha pande zinazoendelea kuhasimiana.
Tangu Aprili 26 mwaka huu, Burundi imetumbukia
kwenye mgogoro wa kisiasa baada ya Rais Nkurunziza kutangaza nia ya
kugombea urais kwa kipindi cha tatu mfululizo.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment