NGUVU ya Umma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kata ya Ruaha, Jimbo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro, wamewavua Uongozi waliokuwa Viongozi wao na kuweka Kamati ya Muda (Task Force), kwa madai ya kuwa Mamluki ndani ya Chama chao.
Waliovuliwa Uongozi na kubaki na Uanachama ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata, George Banda, Katibu, Ally Mponda, Katibu Mwenezi, William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na Mjumbe wa Kamati Tendaji, Mwalimu Myami.
Katika Kikao cha ndani cha Julai 2 (Ukumbi wa Linas), kilichosimamiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mafunzo wa Chadema Taifa, Benson Kigaila; Baada ya kusikiliza ‘Tuhuma’ za Viongozi hao, aliwauliza wanachama wanataka nini, ambapo wote walipaza Sauti; Wavuliwe Uongozi na kubaki Wanachama!.
Aidha Tuhuma zilizoelekezwa kwa Viongozi hao, ni Kuwafukuza Viongozi wenzao Watatu wa Chadema, kwa kutumia Vifungu visivyokuwemo kwenye Katiba ya Chadema, ilihali wakijua ni kukinyang’anya Chadema Ushindi wake halali na kukifurahisha Chama Mapinduzi(CCM).
Nyingine ni Viongozi hao kuhamisha Vikao vya Chama, ambapo badala ya kufanyia kwenye Ofisi ya Chadema Kata, kwa Miezi zaidi ya Minne walihamishia Vikao na Ofisi kwenye Mgahawa wa mmoja wa Viongozi hao kinyume cha Katiba.
Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri kuchaguliwa Mwenyekiti wa Muda kati ya Viongozi waliochaguliwa na Wanachama; Hii ikiwa ni mara tu baada ya kumvua, Banda aliyekuwa Mwenyekiti, ambapo, Joram Zacharia, alithibitisha kuchukua UKatibu aliovuliwa, Mponda.
Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka kuzungumza na Mwandishi hata walipopigiwa simu za Viganjani kuelezea walivypokea kuvuliwa Uongozi na kuwa Wananchama; Aliyekuwa Katibu, Mponda, pekee alikiri kuondolewa, akisema, “Siasa ni Kijiti, lazima tupokezana”.alisema
Hata hivyo, Longa alikiri kupokea Fomu za Viongozi watatu waliovuliwa Uongozi na kubaki Wanachama wa Chadema, Banda, Mponda na Mnunga, ambao wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.
Awali Mponda, alimthibitia Mwandishi wa habari, kuhusu azma yake kutia nia ya kugombea Udiwani wa Kata hiyo wakiwemo Viongozi wenzake waliovulia Madaraka, jambo ambalo limeendelea kuwawatia Shaka Wana Chadema kuwa, huenda kulikuwa na kitu nyuma ya Pazia
0 comments :
Post a Comment