Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe (katikati) akishangilia goli lake kwa kuwapungia mkono mashabiki
Mabingwa wa Tanzania bara Young Africans ‘Yanga’, leo wameibuka na
ushindi mwembamba wa goli 1-0 mbele ya Khartoum Nalitonal Club katika
mwendelezo wa michuano ya Kagame Cup mechi iliyopigwa leo jioni kwenye
dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezo ulianza kwa kasi lakini Khartoum walionekana kuwamudu vyema Yanga
dakika za mwanzoni na walifanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa lakini
hawakuweza kuzitumia vyema nafasi hizo kupachika mabao.
Goli la Yanga liliwekwa kambani na mshambuliaji wao Amis Tambwe dakika
ya 30 kipindi cha kwanza aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona
uliopigwa na Haruna Niyonzima.
Kipindi cha kwanza kilimalizika huku Yanga wakiwa mbele kwa goli moja
wakati Khartoum Naional Club wakiwa hawajapata goli licha ya kupata
nafasi kadhaa za kufunga kwenye kipindi cha kwanza.
Kikosi cha Yanga kilichoanza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Khartoum National Club
Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wamecharuka na kuonekana kusaka
goli kwa udi na uvumba lakini walipoteza nafasi nyingi za kufunga
zilizopatikana. Amis Tambwe, Andrey Coutinho na Simon Msuva walikosa
nafasi nyingi za wazi na kuiokosesha Yanga ushindi wa magoli mengi.
Khartoum walionekana kuzidiwa hasa dakika 15 za mwisho kwani walijikuta
wakishambuliwa muda wote na wao kubaki kuokoa hatari nyingi langoni
mwao.
Kikosi cha Khartoum Kilichoikabili Yanga
Kwa matokeo hayo, Yanga inashika nafasi ya pili kwenye Kundi A
linaloongozwa na Gor Mahia wakati Khartoum wakiwa nafasi ya tatu.
Kutokana na Yanga kushika nafasi ya pili kwenye kundi lake, itakutana na
Azam FC walioongoza kundi C kwenye mchezo wa robo fainali utakaopigwa
siku ya Jumanne kwenye uwanja wa Taifa.
Manahodha wa timu zote mbili wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi kabla ya kuanza kwa mchezo.
CREDIT:SHAFFIHDAUD THE NUMBER 1 SPORT BLOG IN TANZANIA.
CREDIT:SHAFFIHDAUD THE NUMBER 1 SPORT BLOG IN TANZANIA.
0 comments :
Post a Comment