Mwalimu Mkuu akamatwa na TAKUKURU akiomba rushwa ya ngono


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ukombozi manispaa ya Singida, Samwel Juma Kingu (47), amekamatwa na TAKUKURU kwa madai ya kuomba rushwa na baadae kutiwa nguvuni akiwa ndani ya nyumba ya wageni.
Mtuhumiwa Kingu anakabiliwa na makosa mawili ya kushawishi/kuomba rushwa ya ngono na kosa la pili ni kujaribu kupewa rushwa ya ngono wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni.
Mwalimu mkuu huyo wa shule ya msingi, alikuwa akiomba rushwa hiyo kwa mwanamke ambaye Februari, 17 mwaka huu alifika shuleni hapo kumwombea uhamisho mdogo wake wa kiume.
Mwanafunzi huo wa darasa la sita, alikuwa anaomba kuhamia  Temeke jijini Dar-es-salaa kuendelea na masomo.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Singida, Joshua Msuya, alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa Aprili, 5 mwaka huu saa 10 jioni, akiwa ndani ya nyumba ya kulala wageni J.M Ferama chumba kilichopewa jina la simba.
Alisema mwanamke huyo alimwomba kwa muda mrefu uhamisho huo na ndipo mkuu huyo, aliweza kumpa sharti  kwamba wafanye mapenzi kwanza ndipo ampatie uhamisho huo.
“Baada ya hapo, mwanamke huyo alifika ofisini kwetu na kueleza jinsi alivyokuwa akiombwa rushwa ya ngono kwa ajili ya uhamisho wa mdogo wake, tuliweza kuweka mtego na kufanikiwa kumnasa akiwa mtupu akisubiri mwanamke naye avue nguo ili atimize azima yake,” alisema.
Msuya alisema kwa sasa wanaendelea kumhoji na upelelezi ukimalizika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment