Tuesday, July 7, 2015
Nkupamah
blog
Vanessa Mdee anaweza kumfanya Beyonce anune au apate wivu kwakuwa muimbaji huyo wa ‘Nobody But Me’ aliwahi kulivutia jicho la rapper mwenye nguvu zaidi duniani, Sean Carter aka Jay Z.
Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Vanessa alisema yeye
mwenyewe alipokutana na rapper huyo wa ‘Run This Town’, mdomo wake
ulipigwa ganzi kwa muda na maneno kushindwa kumtoka.
“Ooh my God! I was so nervous,” alikumbushia Vanessa.
“Lakini bahati nzuri nilikuwa sim-interview. Halafu mimi nina ugonjwa
fulani hivi, kama nampenda mtu au nam-admire mtu nanyamazaga kimyaa,”
aliongeza Vanessa.
“I was just like…. And he was so nice, he was like ‘ooh my God you’re
so pretty’, like ‘they had to put your face on MTV’. I was like ooh my
God ataniua…sasa sijui hata jinsi ya kujibu ni kama lugha inanipotea.”
Vanessa alidai kuwa Baba Blue Ivy ni mtu poa tofauti kabisa na watu wanavyomchukulia.
“He was so nice, very calm. Nikamkumbusha kwamba walikuja Tanzania…
and he was like ‘yeah Tanzania is a beautiful country’. Yaani very nice
guy, very diplomatic. Halafu hana majidai ya ajabu, labda kwa sababu
mimi nilikuwa back stage and there was nobody in backstage,” alieleza
Vee Money.
Nkupamah blog
0 comments :
Post a Comment