- Nkupamah blog

Mkurugenzi
Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano
kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Bwana Ernest Kimaya.

Mwenyekiti
wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya akizungumza na waandishi
wa habari leo juu ya ushirikiano na kampuni ya Zantel leo. Katikati ni
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose na Mkurugenzi wa Masoko wa
Zantel, Bi Progress Chisenga,

Mkurugenzi
Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari leo juu ya ushirikiano wao na chama cha Maalbino Tanzania. Kulia
ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga, na Mwenyekiti
wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya
Kampuni
ya simu za mikononi ya Zantel leo imekisaidia Chama cha Maalbino
Tanzania katika mpango wake wa kusambaza elimu juu ya ulemavu wa ngozi
kwa jamii pamoja na msaada wa jumla ya shilingi milioni 5 ambao unalenga
kusaidia uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini.
Zantel
kwa kushirikiana na Chama Cha Maalbino kitajikita kutoa elimu hii kwa
kusambaza ujumbe mfupi kwa wateja wake pamoja na kutumia vipindi vyake
inavyodhamini ili kupeleka ujumbe kwa jamii kiujumla.
Pamoja na
hiyo pia, Zantel inajipanga kutumia mikutano ya wafanyakazi pamoja na
matamasha ili kuhakikisha ujumbe kuhusu ulemavu wa ngozi unawafikia watu
wengi zaidi.(VICTOR)
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Pratap Ghose
alisema mchango huo katika kuwawezesha Chama cha Maalbino ni sehemu ya
huduma za kampuni yake kwa jamii.
“Tatizo
kubwa ni ukosefu wa elimu miongoni mwa wanajamii, na kwa hakika hatua
kubwa imepigwa katika kupambana na tatizo hili tayari, na sisi kama
Zantel tunaamini kwa kutumia uwezo wetu kama kampuni ya simu tunaweza
kushiriki kulimaliza tatizo hili la mauaji ya ndugu zetu’ alisema
Pratap.
Kwa
mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu
wa ngozi 5,200 na wengi wao wanaishi kanda ya ziwa, na toka mwaka 2009
jumla ya kesi 155 zinazohusu walemavu wa ngozi zimeripotiwa kwa vyombo
vya sheria kwa mujibu wa taasisi ya Under the Same Sun.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya,
ameipongeza kampuni ya Zantel kwa mchango wao akisema utasaidia sana
katika juhudi zao za kupigania haki za walemavu wa ngozi nchini.
‘Watu
wenye ulemavu wa ngozi ni kama binadamu wengine wa kawaida, hivyo
tunaiomba jamii isiwatenge ndugu zetu hawa’ alisema Kimaya.
Bwana
Kimaya pia aliomba wadau wengine wajitokeze kuwawezesha walemavu wa
ngozi waweze kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo.
“Jamii
yetu ya walemavu wa ngozi ina matatizo mbalimbali, hivyo tunazidi
kuwaomba watu binafsi, serikali pamoja na makampuni mbalimbali wazidi
kujitokeza kusaidia kundi hili la jamii’ alisisitiza Kimaya.
Chama cha
Maalbino Tanzania kilianzishwa mwaka 1978 kikiwa na lengo la kulinda na
kuwezesha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini na kinahudumia zaidi ya
wanachama 1,200.


0 comments :
Post a Comment