CHADEMA MOROGORO WAGANYIWAKA, KATIBU MAZIMBU AJIUZULU

Na Bryceson Mathias, Morogoro

KUPITISHWA kwa Majina ya Viongozi walioshindwa Kura za Maoni ndani ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema) Morogoro, kumekigawa Chama hicho na kusababisha, kujiuzulu nyadhifa zao wakipinga Kukatwa kwa Mshindi wao wa Udiwani wa Kata ya Mazimbu, Ebzyan Mokiwa, na kupewa, Mohamed Kilongo (Butelezi).

Viongozi waliojiuzulu ni pamoja na Katibu wa Kata ya Mazimbu, Mchungaji James Power Mabula, na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee (BAZECHA), Disckson Magambo, waliodai wanajiuzulu kutokana na kutoridhiwa na Maamuzi ya Chadema Wilaya ya Morogoro Mjini.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mchungaji Mabula amethibitisha Kujiuzulu Wadhifa wake wa Ukatibu wa Chadema Mazimbu, akisema kama Mtumishi wa Mungu hawezi kushiriki kuyaishi Maovu na Dhuluma ya aina yoyote ikiwemo Rushwa, isipokuwa kuyakemea kama Maandiko yanavyomuagiza.

“Ni kweli awali nilisema, Nimeitwa kuitumikia Chadema na nitaendelea na kuwa Mwanachama mwaminifu wa Chadema, ila siwezi kushiriki kuwanyima Haki maana, Haki huinua Taifa, dhambi ni aibu ya watu wote, sitaki kubeba dhambi”.alisema Mabula.


Mokiwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa MODECO alikiri kukatwa na Chadema Wilaya na kutoshirikishwa na Timu ya kumnadi Mgombea (Mshindani wake), ambapo yeye alidai, atendelea kuwa Mwanachama na Mwenyekiti wa Mtaa wa MODECO, ila “Nimeumizwa na niliyotendewa”.

Wachambuzi wa Siasa wamesema, Sakata la kukata Majina ya Washindi wa Chadema litakigharimu Chama hicho, na imefahamika kuwa kwenye Kata ya Kihonda Maghorofani, nako Mshindi wao wa Udiwani, Elizeus Rwegasira, alikatwa jina kuwekwa, Gabriel Temba, aliyeshindwa.

Hata hivyo wamedai, CCM imeshajihakikishia Ushindi wa Jimbo la Mvomero kupitia kwa Mgombea wake, Sadiq Murad, hata kama jimbo hilo linaonekana ni Ngome ya Chadema, wanadai kukatwa kwa jina la Mgombea wao aliyegombea Ubunge kwa  Tiketi ya Chadema Mvomero, Matokeo Wodern Mang’eta, aliyeasisi Chama hicho huko na kupewa, Mchungaji Osward Mlay, ni Kigezo kikubwa cha Mtiti huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment