Kundi la watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo
wamevamia na kuibomoa nyumba ya mgombea ubunge wa chama cha wananchi CUF jimbo
jipya la nanyamba wilaya ya mtwara vijijini, twahiri saidi baada ya kushindwa
kurudisha fomu ya ubunge na kutokomea kusiko julikana huku simu zake za mkononi
zikiwa hazipatikani.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya viongozi wa
chama hicho na wanachi wa jimbo la Nanyamba wamesema mazingira aliyotoweka
mgombea huyo yanaonyesha wazi kuna mchezo mchafu umefanywa ili
kutoa fursa kwa mgombea wa CCM Abdallah Chikota kupita bila
kupingwa katika jimbo hilo.
Akizungumzia tukio hilo katibu kata wa CUF kata
ya Milango Minne eneo analotoka mgombea huyo, amesema mwisho wa kuwasiliana na
mgombea huyo ilikuwa majira ya saa saba akimuhimiza kuwahisha fomu kwa
msimamizi wa uchaguzi.
Hata hivyo anasema majibu ya mgombea huyo
yalionyesha wazi kuna jambo baada ya kudai hawezi kuacha ajira yake na kuingia
kwenye kinyang’anyiri cha uchaguzi wakati viongozi wa CUF taifa walimuaidi
kumpa shilingi milioni 30 kwa ajili ya uchaguzi na wameshindwa kufanya hivyo na
baada ya maneno hayo simu zake hazikuweza kupatikana mpaka muda huu.
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya maji
wa nanyamba oscar ng’itu ambaye aliongozana na mkuu wa kituo cha polisi
nanyamba alitembelea nyumba iliyobomolewa na kutoa agizo kwa wananchi kuwataja
watu waliyohusika na tukio hilo vinginevyo mkono wa sheria utachukua mkondo
wake
0 comments :
Post a Comment