IMEBUMBULUKA!
Hatimaye Jeshi la Polisi Tanzania (PT) limeanika picha ya mtu
anayedaiwa ku
wa ndiye mfadhili mkuu wa matukio mbalimbali yanayohusishwa
na ugaidi likiwemo lile la mauaji ya watu saba kwenye Kituo cha Polisi
Stakishari, Dar lililotokea saa 5 usiku, Julai 12, mwaka huu na yale
mapigano ya Amboni, Tanga.
Mtu huyo
aliyetambulika kwa jina la Ally Mtozen Hery ambaye anadaiwa kuishi kwa
kujibadili kama kinyonga kwa muonekano wa sura, wakati mwingine huvaa
mavazi ya kike ili asijulikane kirahisi.
Akizungumza
na Uwazi juzikati, Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman
Kova alisema uchunguzi uliyofanywa na kikosi kazi cha jeshi hilo
umebaini kuwa, mtuhumiwa huyo ana mtandao mpana na ndiye mfadhali mkuu
wa matukio mbalimbali ya uvamizi, mashambulio na uporaji wa silaha
yanayotokea nchini.
Suleiman Kova akionyesha picha ya mtuhumiwa huyo.
Kova
aliongeza kuwa, hivi karibunim Hery amehusika katika kufadhili tukio la
Amboni Tanga, Mkuranga, Stakishari na mengineyo lakini hatimaye jeshi la
polisi kwa kutumia kikosi cha intelijensia kimeweza kubaini nyendo zake
na kuinasa picha yake hiyo.
“Tunachotaka
mtu huyo ajitokeze mara moja na kujisalimisha polisi. Kwani hata
afanyaje lazima tutamkamata tu,” alisema Kamishna Kova.
Akaongeza:
“Ile milioni 50,000,000 iliyotangazwa na IGP Ernest Mangu sasa imefikia
mahala pake kwa mtu atakayeweza kusaidia kupatikana kwa mtuhumiwa
huyo.”
Kova
aliendelea kusema mtuhumiwa huyo wakati mwingine hupenda kutembelea
Pemba, Tanga, Dar na ukanda mzima wa Pwani.Katika mahojiano na Kamishna
Kova alisema hadi sasa, watuhumiwa tisa wanashikiliwa na jeshi hilo
kutokana na tukio la Stakishari.
“Si
vyema kuwataja kwa majina tunaowashikilia kwa sababu za kiupelelezi
lakini hadi sasa kwa jitihada za jeshi letu makini tunawashikilia
watuhumiwa tisa na mahojiano yanaendelea,” alisema Kova.
Mbali na mtuhumiwa huyo kusakwa na jeshi la polisi, mtuhumiwa mwingine aliyekuwa akisakwa na jeshi hilo amejisalimisha polisi akiwa na wake zake wawili na sasa anahojiwa kwa kina.
Mbali na mtuhumiwa huyo kusakwa na jeshi la polisi, mtuhumiwa mwingine aliyekuwa akisakwa na jeshi hilo amejisalimisha polisi akiwa na wake zake wawili na sasa anahojiwa kwa kina.
Aliongeza
kusema mtuhumiwa huyo aliyejisalimisha polisi aliwahi kuwa mtumishi
ndani ya jeshi la polisi lakini alifukuzwa kazi mwaka 1998 kutokana na
kutoeleweka kwa nyendo zake.
Polisi
huyo aliyeachishwa kazi akiwa na cheo cha sajenti anafahamika kwa jina
maarufu la Mzee Mzima ambapo akiwa kazini kitengo cha redio (999)
ambacho hushughulikia matukio ya uhalifu kwa haraka nyendo zake zilikuwa
hazieleweki ndani ya jeshi hilo.
“Hatuwezi
kuvumilia damu za askari wetu zikipotea bure. Ni lazima tuhakikishe
kazi tunaifanya ipasavyo na hao watuhumiwa tisa tunaowashikilia
wanaendelea kutupa taarifa muhimu,” alisema Kova
0 comments :
Post a Comment