Mgombea
urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na
wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa
katika viwanja vya Jangwani mapema leo.Mh Lowassa amesema kipaumbele
chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni
za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa
Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina
Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika
uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani leo.
Mgombea
mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji
akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia
uzinduzi wa Kampeni za Ukawa leo katika viwanja vya Jangwani
Mwenyekiti
wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar
Waliojitokeza katika uzimduzi wa Kampeni za Ukawa zilizofanyika Jangwani
leo.
Mwenyekiti
wa Chadema Taifa, Mh Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akiwa na wagombea
urais kwa Upande wa Zanzibar na Upande Wa Bara na mgombea mwenza bara
wakionyesha Kitabu chao cha Ilani ya Uchaguzi mwaka 2015 katika uzinduzi
wa kampeni za ukawa uliofanyika katika viwanja vya jangwani.
Halima Mdee akihutubia
Wagombea
Ubunge katika majimbo ya Dar Es Salaam wakitambulishwa mbele ya wakazi
wa jiji la Dar waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa Kampeni za
Ukawa leo zilizofanyika katika Uwanja wa Jangwani.
Mgombea
ubunge wa jimbo la Kisarawe kwa tiketi ya CUF Kingwendu akisikiliza
hotuba ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema chini ya Mwamvuli ya Ukawa
Mwenyekiti
wa NCCR Mageuzi, Mh James Mbatia akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la
Dar Waliojitokeza leo katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jangwani
jijini Dar
Waziri
Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Mh Fredrick Sumaye akihutubia wakazi wa
jiji la Dar waliofika katika viwanja vya Jangwani wakati wa uzinduzi wa
kampeni za Ukawa
Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya jangwani leo
Mgombea
Urais kwa tiketi ya Chadema na Mgombea Mwenza wakiwaaga watanzania
waliojitokeza katika viwanja vya jangwani katika uzinduzi wa kampeni za
Ukawa
0 comments :
Post a Comment