Nyomi la Watu katika mkutano wa kampeni.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John
Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma
waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa
Mbeya mapema leo mchana,kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania
ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano,ambapo uchaguzi
unatarajiwa kufanyia Oktoba 25 mwaka huu.
Maelfu ya
Wananchi wa Tunduma waliojitokeza kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe
Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika uwanja wa
shule ya msingin Tunduma mkoani Mbeya.(VICTOR)
Wananchi wakiwa wamefurika katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchama kumsikiliza mgombea urais wa CCM akimwaga sera zake kuwaomba Watanzania wamchague na kumpa ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma mapema leo mchana kwa ajili ya mkutano wa kampeni.
0 comments :
Post a Comment