Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA),Eliud Sanga (
kati kati) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya
Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa(LAPF), akibadilishana mawanzo na Katibu
mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe, ( kulia) ambaye pia ni Meneja wa PPF
Kanda ya Ziwa , Augosti 24, mwaka huu mjini Morogoro baada ya mwenyekiti
huyo kufungua mafunzo kwa wafanyakazi wa mbalimbali wa mifuko yote ya
hifadhi ya jamii chini inayounda Jumuiya hiyo ( kushoto) ni Ofisa
Matekelezo wa Mfuko wa PSPF Makao makuu Dar es Salaam.
JUMUIYA
ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) umewataka vijana
wanaoajiriwa katika mifuko
inayounda jumuiya hiyo kuingiza mawazo mapya
ya ubunifu katika kubuni mbinu mbadala za vivutio ili kukubalika katika
soko katika maeneo ya vijijini ambako huduma hizo hazijawafikia watu
wengi.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa TSSA, Eliud Sanga , Augosti 24,mwaka huu ,
wakati alipofungua mafunzo ya siku tano kwa wafanyakazi mbalimbali wa
kutoka mifuko yote ya hifadhi ya jamii chini inayounda Jumuiya hiyo .
Alisema
kuwa, soko bado ni kubwa la kutatafuta wanachama walio nje ya ajira
isiyorasmi kuwaingiza katika mifuko hiyo hivyo ni vyema wakaanza
kuelekeza nguvu zao katika kutafuta wanachama maeneo ya vijijini ambako
kuna idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji huduma zao.
Mwenyekiti
huyo ambaye pia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi ya wafanyakazi
wa Serikali za Mitaa(LAPF), alisema si jambo jema kuendelea kulumbuna na
kugombania wanachama katika maeneo ya mijini kwani soko bado ni kubwa
maeneo ya vijijini ambapo kuna ajira binasfi na isiyo rasmi.(VICTOR)
Alisema
endapo vijana wasomo wanaoajiriwa katika mifuko hiyo wanaingiza mawazo
mapya na ubunifu wao , kila mfuko utakuwa na hazina kubwa ya wanachama
kutokana na kuwafikia wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini ambao
ni wakulima na wafugaji wenye uwezo wa kuchangia mifuko hiyo.
Mwenyekiti
huyo wa TSSA , alisema kutokana na mifuko hiyo kujikita katika maeneo
ya mjini imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa asilimia nne pekee na endapo
itaongeza juhudi za kuwafikia watu wa maeneo ya vijijini inaweza kufikia
zaidi ya asilimia 96.
Alisema ,
kuna kundi kubwa la wakulima,wafugaji na waendesha bodaboda ambao
mifuko hiyo inapaswa kwenda kuhamasisha kujiunga na kuchangia huduma
hizo za hifadhi ya jamii na pia kuangalia namna ya kutangaza mafao hayo.
Naye
Katibu Mkuu wa TSSA, Meshack Bandawe, alisema malengo ya kuanzisha
Jumuiya hiyo ni kufanya kazi kwa pamoja na kwa lengo moja ili
kuhakikisha sekta ya hifadhi ya jamii inaimarishwa ili kuingiza
Watanzania katika mifuko hiyo na waweze kunufaika nayo.
Mafunzo
hayo ya siku tano yanawashirikisha wafanyakazi kutoka mifuko ya NSSF,
PPF, LAPF, GEPF,NHIF na ZSSF na yamelenga kuwagengea uwezo wa ufahamu
mkubwa juu ya madhumuni, malengo , umuhimu na misingi ya sekta ya
hifadhi ya jamii ili kuboresha utendaji wao wa kazi katika sekta ya
hifadhi ya jamii ili kuwafanya watanzania wengi wafaidike.
Bandawe
ambaye pia ni Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa,alisema kuwa kupitia Jumuiya
hiyo sasa wataanza kuwaelimisha wananchi wote walioko rasmi katika soko
ajira na wale wasio rasmi waweze kukingwa na mifuko ya hifadhi ya jamii .
Alisema
kuwa wanaangalia namna ya kuiboresha mifuko hiyo kwa kupata uzoefu jinsi
mifuko hiyo inavyofanya kazi katika nchi za Afrika mashariki ambayo
imekuwa ikisaidia sana wananchi hasa wanaoishi katika maeneo ya
vijijini.
Katibu
mkuu huyo alisema, kupitia mafunzo hayo wanaangalia namna ya kupata
wanachama ambao ni Watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza kuchangia
kwenye mifuko hiyo wakiwa huko huko na wale wanaoishi maeneo ya
vijijini.
0 comments :
Post a Comment