Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.
Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutano
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa
Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza,
Agrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wake
Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.
Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Suluhu,
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.
Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.
Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.
Na Joachim Mushi, Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema
kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa
halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara
ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na vijana.
Kauli hiyo imetolewa leo na
mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa
akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa
Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na
wananchi wengine.
Akinadi ilani ya CCM alisema chama
hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana
wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa
jiji kukamata biashara za akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki
mjini.
“…Iwapo CCM itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya kufanyanya…hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku,” alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu.

Alisema Ilani ya CCM imepanga
kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana wanapata
ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na kufufua viwanda vilivyosimama
kikiwemo cha ‘General Tyre’ ikiwa ni mpango wa kumaliza tatizo la ajira
kwa vijana.
Aidha alisema mpango mwingine
ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la mikataba ya
ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa, “…Tukifanikiwa kuingia
Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha inafanya
kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari madogo
na makubwa,” alisema Bi. Suluhu.
Aliongeza Serikali ya CCM itaunda
ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji zinakuwa za uhakika kwani Mkoa
wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya watu inakuwa kila uchao.
Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo vya
ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka.
Awali kabla ya mkutano wa Arusha
Bi. Suluhu alifanya mikutano katika majimbo ya Hai, Siha na Arumeru
yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani Arusha. Akiwa
katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi
wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo hayo.Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na vijana

0 comments :
Post a Comment