………………………………………………………………………………….
Na Magreth Kinabo- maelezo
Vyombo vya habari vimeshauriwa
kutoa elimu juu ya usalama barabarani ili kuifanya jamii iweze
kuepukana na ajali ya barabarani badala ya kuripoti idadi ya kujeruhi
watu waliokufa na kujeruhiwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari -(MAELEZO), Assah Mwambene wakati
akitoa mada juu ya uzoefu wa vyombo hivyo nchini Tanzania(Tanzania Media
Landscape) katika masuala ya usalama barabarani kwenye semina ya siku
mbili kuhusu suala hilo inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii uliopo jijini Dares Salaam.
“Vyombo vya habari vinapaswa
kufanya utafiti wa kina pale ajali zinapotokea ili kubaini chanazo cha
ajali hiyo na kutoa elimu kwa jamii badala ya kuripoti idadi ya vifo na
majeruhi pekee. Ikiwa vyombo vya habari vitafanya hivyo vitabadilisha
mitazamo ya watu jinsi ya kuweza kuepukana na ajali hizo ambazo na
vitasaidia kupunguza idadi vifo visivyohitajika na majeruhi
vinavyotokana na ajali hizo,” alisema Mwambene.
Aliongeza kwamba vyombo hivyo
vitoe elimu kwa jamii juu ya ufahamu wa alama za barabarani, jinsi ya
kutumia barabara hasa kwenye vivuko vya watembea kwa miguu vyenye alama
ya pundamilia, kuelimisha watembelea kwa miguu juu ya sheria na kanuni
za usalama barabarani na kutoa waomea aibu watu wanaosababisha ajali
hizo.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema
vyombo hivyo na mitandao ya jamii vina wajibu wa kutoa elimu juu ya
jambo hilo na kulifanya kuwa ni agenda au janga la kitaifa kama
isiposimamiwa vizuri, lakini kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa
habari mfano kutotoa picha za watu waliopata ajali zenye kuumiza na
kuleta hisia mbaya kwa ndugu na jamii.
Kwa upande wake Mratibu wa
shughuli za Usalama Barabarani kutoka Wizara hiyo,Dkt. Mary Kitambi
alisema lengo la semina hiyo ni kuelimisha vyombo hivyo ili viweze kutoa
elimu hiyo kwa jamii.
“ Tumeanzisha mradi huu baada
ya kuona ajili za barabarani zimeongezeka kwa kushirikiana na Shirika
la Afya la Dunia(WHO) ili kutoa mchango wa kusaidia masuala ya usalama
barabarani, ili kuweza kupunguza mzigo kwa Serikali wa kuwahudumia
majeruhi na madhara ya kijamii,’’ alisemaDkt .Kitambi.
Naye Mwezeshaji kutoka WHO,
Mary Kessi alisema utashi wa kisiasa unahitajika ili kuweza kuleta
mabadiliko kwa jamii juu ya suala hilo.
Alisema mradi huo ni wa miaka mitano na unafadhiliwa na Bloomberg Initiative for Global Road Safety (BIGRS) nchini Tanzania.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la
Usalama Barabarani, Inspekta Deus Sokoni aliitaka jamii kuzingatia
sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali hizo.
Aliongeza kwamba asilimia 76 za ajali hizo zinatokana na sababu za kibinadamu, asilimia 16 kiufundi na asilimia 8 kimazingira.
Mwezeshaji wa semina hiyo,
Callie Long kutoka Canada aliwataka waandishi hao kuwa wadadasi pale
ajali zinapotokea ili waweze kubobea katika uandishi wa habari juu ya
suala hilo
0 comments :
Post a Comment