Tuesday, August 25, 2015
@nkupamah blog
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015, kuhakikisha vinafuata na kuheshimu ratiba ya uchaguzi waliyojiwekea.
Katika
taarifa kwa njia ya video iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani amesema kuwa vyama vyote
vilishiriki katika kuandaa ratiba hiyo na kuwa viliiridhia hivyo hawana
budi kuhakikisha wanaifuata.
“Tulikaa
na vyama, mimi sikuamua hii ratiba, wao walipendekeza na wakakubaliana
na wakatoa ratiba hii, cha kwanza kabisa vyama vya siasa wazingatie
waliyoyaweka humu,” alisema Kailima.
Aliongeza kuwa utaratibu huo upo kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Uchaguzi ya 2015 na kuwa wakikiuka, sheria itawakamata.
“Kwenye
maadili (Sheria ya Maadili ya Uchaguzi 2015) kuna eneo ambalo vyama vya
siasa na wagombea wanakubaliana kuzingatia muda wa kuanza kampeni na
muda wa kumaliza kampeni,” alisema.
Aliongeza
kwa chama au wanasiasa watakaokiuka wataitwa kwenye kamati ya maadili
na kuhojiwa na wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Agizo
hilo la NEC linakuja siku chache baada ya CCM kuzindua kampeni zao siku
ya Jumapili katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam ambapo
shughuli hiyo ya uzinduzi ilihitimishwa majira ya saa 12.34 jioni, ikiwa
ni nusu saa zaidi ya muda unaotakiwa kisheria.
0 comments :
Post a Comment