Ukimya
wa miaka miwili wa Nuru The Light ulikuwa na makusudi mahsusi ya kutaka
kubadilisha upepo wa muziki wa Tanzania. Ameutumia kutengeneza muziki
tofauti, mzuri na utakaokuwa na
ladha inayoishi kwa miaka mingi zaidi
kwenye masikio ya wapenzi wa muziki.
Na sasa anarejea kwa kishindo kwa
kuachia wimbo anaouelezea kama wenye utofauti mkubwa na muziki uliopo
kwenye mzunguko wa nyimbo zinazochezwa kwenye redio.
Nuru anasema hakutaka ujio wake
kutoka kwenye ukimya wa miaka miwili uwe wa kawaida na ndio maana
ametumia muda mrefu kutengeneza kazi yake mpya aliyoipa jina ‘L’.
“Hii kazi nimeanza kuifanya tangu
January,” anasema Nuru. “Ni nyimbo ambayo nimeirekodi sana. Nimefanya
nyimbo nyingi lakini zaidi ni nyimbo mbili ambazo nilitaka uwe ujio
wangu mpya.”
Anasema wimbo ‘L’ ndio ulioonekana
kupenya zaidi na kuwa na sifa zote za kutimiza azma yake ya kurejea kwa
mshindo mkuu. “Huu ni ujio mpya, kitu tofauti ambacho mimi kama Nuru
nimewahi kufanya,” amesisitiza muimbaji huyo.
“Nadhani nilitaka kufanya kitu ambacho watu watasema ‘ohh kaja kitofauti tena kama vile nilivyokuja na Muhogo Andazi.”
Muimbaji huyo anaeleza kuwa L ni
herufi iliyo na mambo mengi chanya na ya furaha kwenye maisha yake na
ameitumia kama jina la wimbo kuyawakilisha.
“L inaweza kuwa Love, Life, Light, ni vitu chanya,” anaeleza.
Nuru amedai L ni wimbo
uliotayarishwa nchini Sweden lakini aliamua kuja kuifanyia video
nyumbani chini ya muongozaji mkongwe wa video, Adam.
Hii inakuwa ni video yake takriban ya tano kuwahi kufanya na muongozaji huyo.
“Nakumbuka kabisa video yangu ya
kwanza Walimwengu ilikuwa ni mimi na Adam, tukasafiri tukaenda Zanzibar
na nadhani tulielewa kutoka kwenye siku hiyo na ikawa imekuwa rahisi
kwangu kufanya kazi naye.”
Nuru amedai kinachompa faraja
zaidi ni kuwa pamoja na kutokuwa na kazi mpya kwa kipindi cha miaka
miwili, bado mashabiki wamekuwa wakiwasiliana naye kumuulizia kuhusu
kazi mpya.
“Nina furaha kwamba mashabiki wamekuwa wakisubiri na sasa muda umefika wa wao kuweza kusikiliza wimbo mpya.”
Usikilize wimbo huo wa mapenzi na
wenye mahadhi ya ‘reggae tamu’ ambao bila shaka unajibu la swali la
kwanini anasema huu ni ujio mpya.
0 comments :
Post a Comment