Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akimfariji Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman kufuatia kifo cha mwanaye
Said Mohamed Chande wakati Rais alipokwenda Chumbageni Tanga kuhudhuria
mazishi ya marehemu.
Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande
Othman akiweka udongo katika kaburi la mwanaye Said Mohamed Chande
wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni Tanga leo
jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Said
Mohamed Chande wakati ya
mazishi yaliyofanyika katika eneo la Chumbageni Tanga leo.Marehemu Said
ni Mtoto wa Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman.
Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib
Bilal akiweka udongo katika kaburi la mrehemu Said Mohamed Chande wakati
wa mazishi yaliyofanyika huko Chumbageni Tanga.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal,Jaji Mkuu Mhe.Mohamed
Chande Othman wakiomba dua wakati wa mazishi ya marehemu Said Mohamed
Chande ambaye ni mtoto wa jaji mkuu yaliyofanyika katika makaburi ya
familia huko Chumbageni Tanga leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
akiifariji familia ya Jaji Mkuu Mhe.Mohamed Chande Othman(aliyesimama
pembeni ya Rais) kufuatia kifo cha mwanaye Said Mohamed Chande mjini
Tanga.
(picha na Freddy Maro)
0 comments :
Post a Comment